Uendelevu

Kwetu sisi, uendelevu wa kimazingira na kijamii ni vipengele vya msingi vya kufikia matokeo yanayotarajiwa na vinaendana na mkakati wetu wa ukuaji wa muda mrefu. Sera yetu ya mikopo inatoa kipaumbele kwa miradi inayokuza uendelevu wa kimazingira na kijamii.

Benki ya CRDB hufadhili miradi na biashara zinazoweka wazi mkakati wake wa kusimamia rasilimali za kijamii na mazingira kwa kuwajibika. Tunatumia viwango bora za kimataifa, (ikiwa ni pamoja na Viwango vya Utendaji vya IFC) na kuzingatia mikataba na mikutano ya kimataifa, ambayo imeidhinishwa na serikali za nchi tunazotolea huduma.

Tunatazamia kuwa mabingwa wa uendelevu katika kanda hii na tuna uhakika kuwa na mchango wa kudumu katika masuala ya hali ya hewa. Mkakati wetu wa uwekezaji wa kijamii unalenga kugusa maisha ya jamii zilizo hatarini kwa kuunda na kuwezesha watu watakaoleta tofauti katika jamii hizo.


Idhini ya GCF na fursa

Kundi la Benki ya CRDB limeidhinishwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Hali ya Hewa ya Kijani (GCF) kama wakala wa fedha na mtekelezaji wa miradi ya kijani nchini Tanzania. Tuko mstari wa mbele kutetea miradi inayoendana na mipango ya nchi na tumeidhinishwa kuunda mifumo ya uwekezaji ili kufikia ufadhili ya kifedha kama vile mikopo yenye masharti nafuu, dhamana na usawa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

GCF inaunga mkono juhudi za nchi zinazoendelea katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi, yaani katika kupunguza utoaji wa gesi chafuzi na, kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi na athari zake. Kupitia GCF, Kikundi chetu kinaweza kukusanya mawazo na kutengeneza miradi (yanayoendana na mpango wa nchi) ili kupata ufadhili unaofikia dola milioni 250 kwa kila mradi mmoja.


Ulinzi wa Mazingira na Jamii

Ili kuhakikisha usimamizi madhubuti wa mazingira na kijamii, Kundi lina sera na taratibu zinatekelezwa kwa wakati mmoja na taratibu zetu zingine za uendeshaji na udhibiti wa hatari. Tuna kitengo maalum kinachoitwa Sustainable Finance Unit (SFU) chenye makao makuu yake katika Kurugenzi ya Mabadiliko ya Biashara, ambacho kinasimamia utekelezaji wa miradi ya mabadiliko ya tabianchi kwa kuzingatia sera na taratibu za Kikundi za kijamii na kimazingira na, kwa kuzingatia mikataba ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Mifumo ya Mazingira na Usimamizi wa Jamii (ESMS).

Kama suala la kisera, Kikundi cha Benki ya CRDB kinafadhili miradi na biashara zinazosimamia athari zao za kijamii na kimazingira kwa uwajibikaji. Tunafanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Kijamii (ESIA) kwa kujitegemea kwa kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Tanzania ya 2004 na kanuni zake za EIA & Ukaguzi za 2005 (na Kanuni yake ya EIA iliyorekebishwa na Ukaguzi-marekebisho ya 2018). Tathmini zaidi inafanywa kufuatia mbinu bora za kimataifa zilizopitishwa, hasa Viwango vya Utendaji vya IFC 8 ili kutathmini na kudhibiti athari za kimazingira na kijamii.


Uingizaji wa Jinsia

Kikundi chetu kina mipango mbalimbali inayozingatia jinsia na uwezeshaji. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, tumeendelea kuuupa haki na usawa wa kijinsia kipaumbele kupitia sera ya kina, ambayo inahitaji mpango wa utekelezaji wa kijinsia kwanzia kwenye maandalizi yake hasa ile inayoungwa mkono na UN-GCF. Pia tunaunga mkono kuzingatia jinsia katika kubuni na kutengeneza suluhisho kama vile mipango ya kuweka akiba na mikopo.

Kuhusu uongozi, tuna programu ya ushauri inayoitwa SHE Initiative, inayowasaidia wanawake kufikia malengo yao ya uongozi na kitaaluma.


Mbinu za Kutatua Malalamiko (GRMs)

Tumejifunza mengi katika mapito yetu, mojawapo ni migogoro mingi ya kijamii hutokea wakati wa utekelezaji wa miradi. Kikundi chetu kimepitisha Utaratibu wa Kutatua Malalamiko, unaohakikisha malalamiko yote ya kimazingira na kijamii yanashughulikiwa yanapotokea wakati wa utekelezaji wa miradi hasa inayofadhiliwa na GCF.

Tunaendelea kuboresha mifumo ya malalamiko na usimamizi wa kesi inaendelea kuwa uwazi na malalamiko kutoka kwa jamii zilizo hatarini na wahusika walioathiriwa na mradi yanasikilizwa.


Majukumu ya Mazingira, Afya, Usalama na Kijamii

Benki ya CRDB Group ni balozi wa mazingira na ina mfumo imara wa usimamizi wa mazingira na kijamii. Tumejitolea kusaidia uhifadhi wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia mipango ya Shirika ya Uwekezaji wa Kijamii (CSI) ambayo inaendana na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Kuhusu usalama, tuna idara thabiti ya Usimamizi wa Usalama na Uendelezaji wa Biashara (BCMs), inayosimamia usalama ndani ya Benki, usalama kazini na wakati wa shughuli zetu za kila siku na utaratibu wa mwendelezo wakati wa usumbufu wowote.

Kwa upande wa afya, Kikundi hutoa bima nzuri ya afya na maisha kwa wafanyakazi, wategemezi wao na umma. Pia tunashughulikia masuala yote yanayohusiana na taarifa za afya ya binadamu, ikiwa ni pamoja na mipango ya afya kama vile saratani, majanga, VVU na mitindo hai ya maisha.

Juhudi zetu za kulinda wateja wetu na jamii zilizo hatarini kutokana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi zinaonyeshwa kupitia njia mbalimbali kama vile kufadhili miradi ya upatikanaji wa chakula, maji safi na usafi (WASH). Pia tunafanya kampeni za uhamasishaji kwa wafanyakazi na jamii juu ya shughuli endelevu.

Pia tunahakikisha Tathmini sahihi ya Athari kwa Mazingira na Kijamii (ESIA) unafanywa kwa miradi yote tunayofadhilii. Zaidi ya hayo, SFU ina jukumu la kuelimisha na kujengea uwezo wafanyakazi wa idara ya mikopo na wahusika wote namna ya kufanya ESMS kwa ufanisi.

  • Mfuko wa Kijani wa Benki ya CRDB Uliidhinisha Mradi wa Kutayarisha Mradi (PPF) kwa Mpango wa Usambazaji wa Teknolojia ya Kukabiliana na Hali ya Hewa ya Kilimo Tanzania - Pakua
  • Mfumo wa Sera ya Makazi mapya ya Benki ya CRDB kwa ajili ya Kukabiliana na Hali ya Hewa ya Kilimo - Pakua
  • Mfumo wa Sera ya Makazi Mapya – Pakua
  • Mfumo wa Usimamizi wa Mazingira na Kijamii wa Benki ya CRDB wa Kukabiliana na Hali ya Hewa ya Kilimo - Pakua

Unaweza kupendezwa na