Benki ya CRDB yawazawadia washindi wa Simbanking bajaji na pikipiki

By: Niels Malangalila | Blog | Machi 19, 2024 01:00

Dar es Salaam. Tarehe 14 Machi 2024: Wateja watatu wa Benki ya CRDB leo wamekabidhiwa zawadi zao baada ya kuibuka washindi kutokana na kufanya miamala mingi ya huduma za benki kupitia simu zao za mkononi maarufu kama Simbanking. Akikabidhi zawadi hizo jijini hapa, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili amesema huu ni mwanzo tu kwa wateja wa benki hii kujinyakulia zawadi katika promosheni ya mwaka mzima ya Benki ni Simbanking yenye kaulimbiu ya Swahiba – lako, langu.

Adili amesema teknolojia imerahisisha mambo mengi hivi sasa kwa kuwawezesha wateja kupata huduma kupitia majukwaa tofauti zikiwamo simu za mkononi ambazo kwa Benki ya CRDB wanayo Programu ya Simbaking inayowaruhusu kupata zaidi ya asilimia 95 ya huduma zake mahali popote walipo. “Simbanking imedumu sokoni kwa zaidi ya miaka 15 sasa, ni njia rahisi ya kupata huduma za Benki ya CRDB na kwa sasa tunayo kampeni ya kuwahamasisha wateja wetu na wananchi kwa ujumla kuitumia na wale wanaoitumia zaidi tunawapa zawadi za aina tofauti. Leo tupo hapa Chanika kukabidhi bajaji moja na pikipiki kwa washindi wetu waliopatikana katika droo ya kwanza ya kila mwezi,” amesema Adili. Waliokabidhiwa zawadi hizo ni Adam Salehe Rashid aliyejishindia bajaji pamoja na Kibwana Hussein Killongo na Rahma Abdul Kyalumbika walioshinda pikipiki kila mmoja. Kukabidhiwa kwa zawadi hizo kunawakumbusha wateja wengine wa Benki ya CRDB kuendelea kutumia Simbanking hali itakayowaweka kwenye nafasi ya kushinda pikipiki au bajaji nyingine zitakazokuwa zinatolewa kila mwezi au Toyota Dualis itakayoshindaniwa kila baada ya miezi mitatu.

“Washindi hawa watatu wa kwanza wamefungua pazia kwa mwaka huu. Naomba mfahamu kwamba kuna magari manne aina ya Toyota Dualis yanayoendelea kushindaniwa hivyo nawasihi wateja wetu na Watanzania ambao hawatumii huduma zetu basi wafungue akaunti kwani kwa kufanya hivyo tu watakuwa wanaingia kwenye droo ya kushinda moja kati ya zawadi nyingi tulizonazo,” amesema Adili.

Ili kushinda moja ya zawadi zinazotolewa na Benki ya CRDB, mteja anatakiwa kufanya miamala mingi kupitia Simbanking kama vile kulipia bili za umeme na maji, kukata tiketi ya usafiri wa ndege, kulipa ada na michango ya shule, kulipia bidhaa zinazouzwa mtandaoni au kununua muda wa maongezi na huduma nyingine nyingi zinazopatikana ndani ya Programu ya Simbanking. “Sifa zilizowapa ushindi wateja hawa watatu zinawezekana kwa mteja mwingine yeyote wa Benki ya CRDB hivyo niwahimize wateja wetu wote kutoka mahali popote walipo kuendelea kutumia huduma za Simbanking ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda zawadi kemkem tulizonazo,” amesema mkuu huyo. Akipokea pikipiki yake, Rahma amesema ataifanya bodaboda ili imwingizie kipato. “Naamini haitonifaidisha peke yangu. Dereva atakayekuwa anaiendesha naye atapata kitu cha kuisaidia familia yake. Nimefurahi kushinda na naipenda zaidi Benki ya CRDB kwani inarudisha sehemu ya faida yake kwetu,” amesema.

Nini Kipya?

...
BLOG
Benki ya CRDB yakabidhi bajaji, pikipiki kwa washindi wa Simbanking

Siku ya Jumatano ya Julai 12,2023 tuliandamana kutoka kwenye kitovu cha barabara ya Msimbazi Kariako...

Soma Zaidi
...
BLOG
Kupambana na changamoto za uviko ili kuwahudumia wateja wetu

Jitihada mpya za mauzo zilisababisha ufanisi wa rekodi uliopatikana mwaka 2020. Amana za reja reja z...

Soma Zaidi
...
BLOG
Benki ya CRDB yafanya mkutano wa kwanza kwa wanahisa mtandaoni, na imetoa utendakazi upya

Wanahisa kwa kauli moja waliidhinisha malipo ya gawio la fedha taslimu shilingi 17 kwa kila hisa, am...

Soma Zaidi