Bima ya Majanga Yote

Maelezo

Bima hii inahusisha mali iliyokatiwa bima eneo lolote kwa mujibu wa taarifa iliyopo katika maelezo ya bima ya awali. Ina husisha Moto, Wizi na majanga mengine kama vile matatizo kutokana na sababu za kiufundi au majanga yanayosababishwa na umeme. Bima hii ni muhimu kwa vifaa vya maofisini kama Komputya, mashine za Vinakilishi (photocopiers), Vikokotozi (calculators),Nukushi (Fax) na nyinginezo.

Bima ya Mkandarasi (CAR) & Bima ya Kiwanda (PAR)

Aina hii ya bima inatoa fidia kwa wakandarasi kutokana na majanga ambayo yanaweza kusababisha hasara katika eneo la kazi kutokana na majanga ya Moto,Tetemeko na madhara mengine kabla ya mradi husika kumalizika.

Aina hii ya bima inatoa fidia kwa wakandarasi kutokana na uharibifu wa mashine hususani vifaa vinavyohamishika kama vile Vijiko/Makatapila (excavators), Magreda, Malori na kadhalika. Washirika katika usafirishaji hawahusiki katika bima hii wanapokuwa katika barabara za umma.

Unaweza kupendezwa na