Internet Banking

Maelezo

Internet Banking inakuwezesha kuwa karibu na akaunti yako, ambapo unaweza kupata taarifa kwa urahisi na kufanya miamala salama na kwa haraka zaidi,masaa 24.


  • Malipo ya mkupuo - sasa unaweza kufanya miamaa hadi 2000 kwa mara kwenda akaunti za CRDB na akaunti zingine za benki ndani ya Tanzania, Pamoja na mitandao ya simu (Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money na Halopesa)
  • Kutuma pesa - Tuma pesa kwenda akaunti zako mwenyewe, akaunti zingine za Benki ya CRDB, fanya malipo ya Kimataifa kupitia SWIFT na Benki za ndani ndani ya Tanzania kupitia TISS
  • Fanya miamala kwenda sarafu za nchi nyingine, (yaani TZS TO FX, FX TO FX, FX TO TZS), Miamala hii yote inaweza kufanywa kupitia viwango vilivyoidhinishwa na bodi au viwango maalum kwa mazungumzo.
  • Unaweza kufanya malipo ya bili ukiwa popote muda wowote. Lipia bili za Serikali (GEPG), malipo ya tiketi za ndege, LUKU, MAJI, Ving'amuzi, kodi za TRA,
  • Tuma pesa kwenda mitandao ya simu (Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money na Halopesa)

  • Kuwa karibu na akaunti yako masaa 24
  • Okoa muda na gharama kwenda tawini
  • Pata huduma ya uhakika na salama
  • Usalama ulioboreswa kupitia uthibitisho wa hatua mbili, kutumia jina la mtumiaji na Nenosiri ama Simu ya OTP, SMS OTP au kifaa cha CRDB.
  • Inaruhusu mtumiaji zaidi ya mmoja
  • Unaweza kuweka viwango mbalimbali vya kufanya miamala

Tembelea tawi la karibu na kitambulisho chako (NIDA, Kadi ya Mpiga Kura, Passport au Leseni ya udereva) ikiwa upo ndani ya Tanzania. Kama upo nje ya nchi bofya hapa kujiunga.

Unaweza kupendezwa na