CRDB Wakala

Maelezo

CRDB Wakala ni wakala wa Benki ya CRDB chini kitengo cha idara ya wateja wadogo. Tumekua mbele kiubunifu katika utoaji huduma za kifedha nchini kwakua Benki ya kwanza kuanzisha huduma ya uwakala nchini Tanzania mwaka 2013 iliyokua ikijulikana kama “Fahari Huduma Wakala”.

CRDB Wakala ni wakala wa kibenki waliopitishwa na kufundishwa utoaji huduma za kifedha kwa niaba ya Benki ya CRDB kulingana na kanuni na mwongozo wa Benki kuu ya Tanzania. Mtandao wa CRDB Wakala unawawezesha watanzania wote walio wateja na wasio wateja wa kibenki kupata huduma zetu za kifedha kiurahisi popote walipo.

Huduma zinazopatikana kwa CRDB Wakala

  • Maulizo ya salio na taarifa fupi za kibenki.
  • Kuweka pesa kwenye akaunti yoyote ya CRDB bila makato yoyote.
  • Kutoa pesa kutoka kwenye akaunti ya CRDB kwa kutumia kadi yoyote ya CRDB au SimBanking ( App au kwa kupiga *150*03#).
  • Malipo ya huduma mbalimbali kama bili ya LUKU, maji, tiketi za kusafiria, ving’amuzi, muda wa maongezi na mengine.
  • Malipo ya Ada za shule.
  • Malipo ya mikopo, ustaafu na huduma za kijamii.
  • Malipo ya Serikali kupitia namba za malipo ya GePG na TRA.
  • Kufungua akaunti mpya ya CRDB papo hapo.
  • Kujisajili kupata TemboCard


Faida ya CRDB Wakala kwa mteja ni kama yafuatayo

  • Okoa Muda : Huduma za mawakala wetu hazina foleni hivyo ni haraka zaidi na kwa uhakika
  • Okoa Gharama : Tumekuondolea hitaji la kwenda umbali mrefu kupata huduma zetu za kifedha, sasa imekua rahisi zaidi mtaani karibu na makazi ya watu.
  • Ongezeko la muda wa huduma za kibenki : Tofauti na matawini ambapo kuna muda malumu wa utoaji huduma, CRDB Wakala inatoa huduma takati wowote.
  • Ujuzi wa huduma za kibenki : CRDB Wakala kama mabalozi wetu wanashiriki katika utoaji maarifa ya huduma zetu na bidhaa kwa wateja.
  • Mawakala wetu kwa njia ya kukubali amana ya pesa wanapunguza hatari kwa wateja wetu wanaotamani kuweka amana kabla ya kusafiri.
  • Mtandao wetu mpana wa CRDB Wakala wenye zaidi ya mawakala 14,000 umetusaidia kufika kila kona ya Tanzania.

Benki ya CRDB pia imekubaliana na Shirika la Posta Tanzania kuwa mmoja wa mawakala wetu kwa kuturuhusu kutumia maduka yao nchini kote kutoa huduma ya CRDB tangu 2013.


Unaweza kupendezwa na