Mkopo wa Jijenge

Maelezo

Miliki nyumba ya ndoto zako

Je, unataka kujenga, kununua au kukarabati nyumba yako? Jijenge Loan ndiyo njia ya kumiliki nyumba ya ndoto zako. Pata mkopo wa Jijenge kutoka TZS Milioni 20 - Bilioni 1 kwa riba nafuu ya 17% na muda wa marejesho wa hadi miaka 20. 

Unaweza kuchukua Mkopo ya Jijenge kwa ajili ya uwekezaji na uhamisho wa mikopo na urejeshaji wa mkopo huu unaweza kufanywa kupitia malipo ya awamu ya kila mwezi au kwa mkupuo - awamu moja baada ya kupokea mkupuo uliopangwa awali k.m. faida za mwisho.

Sifa 6 za Mkopo wetu wa Jijenge

  • Unatolewa kwa Watanzania wote wenye umri wa miaka 21-60; waliojiriwa, waliojiajiri na wanaoishi nje ya nchi.
  • Mkopo huu unatolewa kwa fedha za Kitanzania pekee.
  • Kiwango cha juu cha mkopo ni shilingi bilioni 1.
  • Marejesho ni hadi kipindi cha miaka 20.
  • Malipo sawa ya kila mwezi - kiasi sawa cha pesa kinachopaswa kulipwa kila mwezi ndani ya muda wa mkopo.
  • Malipo ya mkupuo - Urejeshaji wa mkopo baada ya kupokea risiti inayoonyesha kiasi kikubwa cha pesa ulicholipwa.

Sababu 7 za kutuma maombi

  • Fursa ya kumiliki nyumba ya ndoto zako ndani ya muda mfupi.
  • Pata mkopo hadi asilimia 90 ya manunuzi au gharama za ujenzi wa nyumba.
  • Kiwango kizuri/nafuu cha riba.
  • Pata amani ya akili na moyo kwa kulipa kidogo kidogo hadi miaka 20. 
  • Uwezekano wa kumaliza mkopo mapema kwa kubadili kiwango cha kulipa kila mwezi. Mfano: mshahara kubadilika. 
  • Dhamana (ikitokea tukio la kifo au ulemavu wa kudumu).
  • Uwezekano wa kununua mkopo wa nyumba kutoka Benki nyingine. 

Ili kutuma ombi, unahitaji…

  • Nakala ya kitambulisho cha Uraia au hati ya kusafiria..
  • Picha mbili za ukubwa wa pasipoti.


ii. Nyaraka zifuatazo (ikiwa umeajiriwa)

  • Barua ya utambulisho kutoka kwa mwajiri
  • Hati za malipo zilizoidhinishwa za miezi 6 iliyopita
  • Taarifa ya benki ambapo mshahara hulipwa kwa miezi 6 iliyopita


Ikiwa Umejiajiri

  • Ukaguzi wa mahesabu wa muda wa miaka 3
  • Taarifa ya mtiririko wa fedha, matumizi (balance sheet) na faida na hasara ya akaunti mwa muda wa miaka 3
  • Taarifa ya benki yoyote (Bank statement) kwa muda wa miezi 12 iliyopita
  • Taarifa kamili kuhusu madeni na amana nyingine zilizotokana na taasisi nyingine.
  • Kwa wateja waliopo nje ya Tanzania


Kwa Wateja wa Tanzanite

  • Nakala ya kibali cha kufanya kazi nchini
  • Mkataba wa kazi au barua kutoka Wizara ya Mambo ya Nje (kitengo kinachosimamia waajiri kutoka nje)


Jinsi ya kuomba mkopo wa Jijenge

  • Tembelea tawi lolote la Benki ya CRDB kote nchini na uulize kuhusu Jijenge.
  • Pakua fomu ya maombi ya Jijenge hapa, chapisha, jaza fomu na urudishe katika tawi lolote la Benki ya CRDB.

Unaweza kupendezwa na