Wateja Maalum

Maelezo

Kitengo cha Wateja Maalum ni cha kipekee, kinachokidhi mahitaji ya wateja maalum na wenye mapato makubwa. Ni huduma inayompa mteja fursa ya kutimiza malengo na mataraji yako ya huduma za benki.


1. Huduma mahususi kwako

Utapokea huduma Bora kutoka kwa meneja husika katika matawi yaliyo na vitengo vya wateja maalum na katika eneo maalumu.


2. Unrivalled convenience – Furahia huduma bure

Katika vituo vyenye hadhi ya Premier Lounges

Kwa umakini unaostahiki, kupitia maeneo matawi mbalimbali ya benki ya CRDB

Kadi yako ya Tembo Card Visa Gold Premier inawezwa kuunganishwa hadi akaunti nne,itakayotumika katika ATMs zote za CRDB na katika vituo vya mauzo(POS),kitaifa na kimataifa

  • Unaweza kutoa fedha taslimu hadi kufikia shilingi milioni 5 kwa siku kupitia ATM. Kiasi hiki cha fedha kinaweza kuongezwa kwa maombi rasmi kimaandishi
  • Muda wa huduma umeongezwa katika vituo vya Premier kuanzia –Jumatatu- Ijumaa kuanzia saa 08:30 (Asubuhi) -05:00 (Jioni) na Jumamosi kuanzia 08:30 (Asubuhi) – 02:00(Mchana)
  • Huduma hadi mlangoni kwa makubaliano maalumu. Wateja waPremier katika vituo vya Premier wanapewa huduma hadi katika ofisi zao au nyumbani kwa bidhaa zisizohusisha fedha taslimu


3. Huduma zinazohusu malipo ya mwisho wa mwezi

Kwa mpangilio maalumu,vituo vinavyotoa huduma ya Premier(Wateja Muhimu)vitafanya miamala ya malipo ya bili za mwezi kama DSTV, bili ya huduma za maji na umeme na karo ya shule.


4. Huduma za kibenki za familia

Huduma zinaweza kutolewa hadi kufikia ngazi ya familia (mfano wanaokutegemea au watoto). Wanafamilia wataunganishwa na huduma hii katika vituo vya Premier na hawatawekewa kikomo katika kufanya miamala.


5. Zawadi Mahususi

Ukiwa na huduma ya Premier,una nafasi ya kuzawadiwa kulingana na thamani ya miamala uliyoifanya kama vile:

  • Kadi maalumu ya Premier / Visa Gold Card
  • kitabu cha cheki kilicho na nembo ya Premierk
  • SIMBanking Facility
  • Internet Banking Facility
  • Utapata punguzo ukitumia kadi ya Premier katika baadhi ya mahoteli.
  • Taarifa kamili ya miamala kupitia mtandao
  • Unafuu wa kupata mkopo yenye riba nafuu
  • Unafuu maalumu wa riba katika miamala yenye malengo maalumu kwa wakati uliopangwa.
  • Unafuu wa huduma muhimu za bima
  • Usimamizi wa mali