Fahad Soud Hilal wa Tanga Anyakua Toyota IST Kupitia Kampeni ya Benki ni Simbanking ya CRDB
By: Niels Malangalila | Blog | September 22, 2025 08:13

Mfanyabiashara na mkazi wa Tanga Mjini, Fahad Soud Hilal aliyeibuka mshindi katika droo ya Agosti ya kampeni ya Benki ni Simbanking ya Benki ya CRDB, amekabidhiwa gari aina ya Toyota IST jijini Dar es Salaam. Hilal amesema amekuwa akitumia huduma za Simbanking kwa muda mrefu lakini sasa umekuwa muda sahihi kwake kuibuka mshindi wa promosheni hii inayoendeshwa na Benki ya CRDB kwa mwaka mzima. “Mimi ni mfanyabiashara. Ninayo malori yanayopeleka mizigo nje ya nchi kama vile Rwanda, Zambia na Congo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo). Mambo yangu mengi ya uendeshaji wa biashara nayakamilisha kwenye Simbanking iwe ni kulipia mafuta, matairi, gharama za vibali vya kuvuka mpaka wa mataifa kwa dereva na msaidizi wake vyote navifanya kwa Simbanking,” amesema Hilal. Kuibuka kwake na ushindi kumemfurahisha Hilal ambaye amewashauri Watanzania wengine kuendelea kutumia huduma za Simbanking anazosema sio tu zinampa muhusika muda wa kutosha kufanya mambo mengine kwa kutolazimika kwenda tawini bali miamala inafanyika kwa urahisi na unabaki na risiti zinazotoa ushahidi wa malipo kama itahitajika kufanya hivyo. Hilal anayeishi na kufanya biashara zake jijini Tanga ameipokelea zawadi jijini Dar es Salaam ambako anayo makazi pia. “Mimi naishi kotekote – Tanga na Dar es Salaam. Nilichagua kuipokelea zawadi yangu hapa Dar es Salaam,” amesema Hilal. Akikabidhi zawadi hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili amesema siku zote wamekuwa wakibuni na kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja wao na jamii nzima kwa ujumla kwani wanaamini huduma bora na za kisasa ni muhimu katika kuimarisha kipato cha mtu binafsi na kuchangia katika maendeleo ya Taifa kwa ujumla. “Tukiitumia kaulimbiu yetu ya Benki inayomsikiliza mteja, tunatumia fursa za maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani kubuni mifumo ya kisasa ya huduma ikiwamo SimBanking kuhamasisha ujumuishaji wa wananchi katika huduma za fedha na uchumi rasmi. SimBanking ni programu inayoongoza kwa kutumiwa na watu wengi nchini lakini tunaendelea kuwahamasisha ili tuwe sehemu muhimu ya kuwaingiza Watanzania kwenye uchumi wa kidijitali,” amesema Adili. Simbanking ni kati ya huduma bora za Benki ya CRDB iliyoanzishwa mwaka 2011, ikiwanufaisha mamilioni ya Watanzania kwa kuwapa huduma kwa saa 24 wakiwa mahali popote. Benki ya CRDB inaendesha kampeni ya Benki ni Simbanking kwa mwaka mzima ikiwazawadia washindi wanaopatikana zawadi za aina tofauti kama vile fedha taslimu, simu za mkononi pamoja na kompyuta mpakato. “Leo imekuwa ni siku ya bahati kubwa kwa ndugu yetu, kaka Fahad Soud Hilal ambaye leo tunamkabidhi gari aliloshinda katika kampeni yetu ya Benki ni Simbanking. Kama ilivyo kwa mshindi aliyetangulia, Fahad naye tunamkabidhi zawadi ya gari aina ya IST ya kisasa tuliyoikatia bima kubwa na kuijaza mafuta ‘full tank,’” amesema Adili.
What's new?


BLOG
CRDB Bank Invites Tanzanians to Seize Green Bond Opportunities for Environmentally Friendly Projects
...
Read More