Uongozi wetu
Benki ya CRDB na Kampuni zake tanzu zinaamini katika watu wake. Ni heshima kubwa kwetu kubeba jukumu la kuongoza kusaidia mamilioni ya watu ukanda wa Afrika Mashariki kukidhi mahitaji yao ya kifedha. Kadri tasnia ya fedha inavyoendelea kukua, mahitaji ya wateja wetu yanakua na sisi pia tunaendelea kukua. Jambo muhimu ni kuwa tumesaidia kuunda na kuelimisha jamii maana ya huduma za kifedha katika maisha ya kila siku na kusaidia mamilioni ya ndoto. Bidhaa, huduma, mawazo na utoaji wetu sasa unagusa maisha ya mamilioni ya watu kila siku. Tunajivunia nguvu na uvumilivu wetu kutokana na mbinu thabiti za kusimamia biashara yetu, na kukidhi matakwa ya watu wetu.