Wekeza kwenye
CRDB Al Barakah Sukuk

Wekeza kuanzia TZS 500,000 au USD 1,000 kwa muda wa miaka 5 kwenye uwekezaji unaozingatia Misingi ya Sharia (Ijarah) na upate faida isiyobadilika

Tanzanian Shillings

TZS 12%

Faida kwa Mwaka

US Dollar

USD 6%

Faida kwa Mwaka

Kwa Nani

Chaguo la uwekezaji linaloendana na maadili ya
kifedha ya Kiislamu

Watu Binafsi
Wekeza kwa usalama, faida thabiti na kwa kuzingatia maadili ya kifedha ya Kiislamu.

Idhini kwa watu binafsi (umri wa miaka 18+), watoto kupitia mlezi, na vikundi.
Makampuni/Taasisi
Chaguo la uwekezaji lenye uwajibikaji wa kijamii, linaloendana na sera za fedha zisizo na riba.

Inafaa kwa makampuni na taasisi zinazofuata misingi ya Sharia.

Faida Kuu za CRDB Al
Barakah Sukuk

Sharia-Compliant (Ijarah)

Inafuata miongozo ya Sharia; imepitiwa na washauri huru wa Sharia.

Mapato Thabiti

Mgao wa faida kila robo mwaka katika kipindi chote cha uwekezaji.

Urahisi wa Uwekezaji

Kupitia SimBanking App au kupitia matawi/fomu za maombi.

Uwezekano wa Uuzaji

Unaweza kuuza kwenye DSE kulingana na uhitaji wa soko kabla ya ukomo.

Hakuna Zuio la Kodi

Unaendelea kupokea faida yako bila makato ya zuio kwenye kuponi.

Kuendeleza Fedha za Kiislamu

Mapato yanasaidia shughuli na bidhaa zinazozingatia Sharia.

Kikokotoo cha Faida

Hesabu Faida yako ya Kila Kipindi

Kumbuka: Hakuna kodi ya zuio kwenye kuponi zako. Mfano unaonesha mgao wa robo mwaka kulingana na kiwango cha TZS 12% p.a.

TZS 12% p.a. | USD 6% p.a.
0%
Kipindi Faida Kabla Ya Kodi Kodi Faida Baada ya Kodi
Kila Robo Mwaka -
Kila Nusu Mwaka -
Kila Mwaka -
Baada ya Ukomo (Miaka 5) -

Muhtasari wa Utoaji

CRDB Bank Plc kupitia
CRDB Al Barakah

Offer Snapshot

Mtoaaji:
CRDB Bank Plc kupitia CRDB Al Barakah
Muundo wa Sukuk:
Ijarah (upangishaji mali)
Kiasi cha Utoaji:
TZS 30,000,000,000 na USD 5,000,000
Muda wa Uwekezaji:
Miaka 5
Faida kwa Mwaka:
TZS 12% • USD 6% (hulipwa kila robo mwaka)
Kiwango cha Chini:
TZS 500,000 au USD 1,000

Tarehe Muhimu

Kufunguliwa kwa Ofa:
9 Agosti 2025
Kufungwa kwa Ofa:
12 Septemba 2025
Kuanza Kutosha Faida:
8 Oktoba 2025
Kusajiliwa DSE:
17 Oktoba 2025
Ukomo wa Uwekezaji:
8 Oktoba 2030
Tarehe za Mgao wa Faida:
8 Jan | 8 Apr | 8 Jul | 8 Oct

Anza Kuwekeza

SimBanking App

  1. Fungua/Pakua SimBanking App (Play Store / App Store)
  2. Ingia kwa namba ya simu/jina la mtumiaji na PIN/nenosiri
  3. Kwenye menyu kuu, gonga Miniapps > Investment/Uwekezaji
  4. Chagua "Al Barakah Sukuk" > "Invest Now/Wekeza"
  5. Weka kiasi (TZS au USD) unachotaka kuwekeza
  6. CDS: Chagua "Sina" kama huna, mfumo utakutengenezea
  7. Hakiki taarifa zako na chagua akaunti ya malipo
  8. Pokea risiti - hifadhi kwa kumbukumbu

Fomu ya Maombi

Pakua Fomu

Pakua fomu ya maombi kutoka tovuti au chukua kwenye tawi la CRDB

Jaza na Wasilisha

Jaza fomu kwa makini na uiwasilishe kwenye tawi la karibu

Uuzaji/DSE

Baada ya kutolewa, unaweza kununua/kuuza kupitia mawakala waliothibitishwa

Pakua Fomu ya Maombi

Maswali ya Mara kwa Mara

Barua Pepe

[email protected]

Namba za Simu

+255 (22) 219 7700

+255 (0) 714 197 700

+255 (0) 755 197 700

0800 008 000 (Bila malipo)

Hati fungani zinazofuata misingi ya Sharia; zinawakilisha umiliki wa mali/manufaa, si deni la riba.

Ni Kwa Nini Uchague
CRDB Al Barakah Sukuk?

Ni uwekezaji wa kipekee unaokuruhusu kupata faida thabiti huku ukizingatia misingi ya kifedha ya Kiislamu. Mapato yako yanadhaminiwa na haitatembea, na unaweza kuuza wakati wowote ule kwenye soko la hisa.