Akaunti ya Biashara

Maelezo

Akaunti ya Biashara ya CRDB ni akaunti mahususi ya hundi kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na wa kati wanaofanya biashara kama mtu mmoja mmoja, kampuni, taasisi au vikundi vilivyosajiliwa. Akaunti hii husaidia wateja wetu kuweka akiba zao za biashara na kufanya miamala ya kibiashara kwa unafuu.

  • Akaunti hufunguliwa kwa kutumia sarafu ya nyumbani (TZS) na za kimataifa(USD/GBP)
  • Kiwango cha chini cha kufungulia ni TZS 20,000/= au 5 USD| GBP
  • Kiwango cha chini cha kuendeshea akaunti ni TZS 20,000/= 5 USD| GBP
  • Akaunti hutumia TemboCard Visa au TemboCard MasterCard.
  • Unaweza kufanya miamala kwa njia mbali mbaili za kidijitali kama SimBanking, Internet Banking, Lipa Hapa (TANQR) and POS machine ( machine za kuchanja).
  • Mteja anaweza kupatiwa kitabu cha hundi.
  • Akaunti hii inaweza kufunguliwa kwa misingi ya Imani ya kiislam (Al Barakah Banking).

  • Akaunti inafunguliwa kwa safari mbalimbali
  • Viwango rahisi vya kufungua na kuendesha akaunti
  • Kupata fursa ya bidhaa za hazina na mitaji
  • Kutoa na kuweka fedha sehemu yoyote katika matawi ya Benki ya CRDB
  • Kutoa pesa kwa sarafu yoyote duniania sehemu yoyote
  • Uhuru wa kufanya miamala kwa njia za kidijitali katika mifumo ya SimBanking (hadi TZS Milioni 20 kwa siku), Internet Banking, Lipa Hapa (TANQR), POS machine(machine za kuchanja)
  • Kupata Bima ya Maisha (KAVA Assurance) ya hadi Sh 5 milioni ikiwa mteja amefariki.
  • Kupata mikopo rahisi ya kuendesha biashara na uwekezaji wa kibiashara kwa riba nafuu
  • Kupata dhamana ya benki (bank guarantees) zinazofanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa wakandarasi na wazabuni
  • Fursa ya kupata mafunzo ya biashara yatolewayo na benki ya CRDB kupitia warsha na makongamano mbalimbali nchini na nje ya nchi
  • Fursa ya kuunganisha mifumo wa malipo na benki (system integration) inayorahisisha malipo kupitia control number kwa huduma mbalimbali kama hospital, shule n.k.

Kufungua akaunti hii ni rahisi, tembelea tawi lolote la Benki ya CRDB lililo karibu nawe popote pale nchini.

Kwa mfanyabiashara binafsi 

  • Barua ya maombi
  • Cheti za usajili wa biashara
  • Taarifa ya msajili
  • Leseni ya biashara
  • Cheti za TIN namba
  • Picha mbili za ukubwa pasipoti
  • Kitambulisho (NIDA, kadi ya mpiga kura au Pasipoti).

Kwa makampuni

  • Barua ya maombi
  • Muhtasari wa bodi kufungia akaunti
  • Nyaraka za usajili wa kampuni
  • Leseni ya biashara
  • Namba ya mlipa kodi
  • Picha mbili za watia sahihi na vivuli vya vitambulisho vinavyokubalika.

Viambatanisho vya ziada

Kwa makampuni ya kigeni:-

  • Cheti cha msajili wa makampuni;
  • Cheti cha usajili kutoka kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC)

Unaweza kupendezwa na