Akaunti ya Tanzanite
Maelezo
Je wewe ni mtanzania unayeishi ughaibuni na ungependa kuweka akiba au kuwekeza nyumbani na kupata ukaribu na wapendwa wako kifedha? Akaunti ya Tanzanite ndio suluhisho lako. Akaunti hii ni maalumu kwa ajili ya watanzania wanaoishi nje ya nchi, inayowasaidia kuweka akiba, kuwekeza na kukidhi majukumu binafsi, kikazi au ya masomo kwa urahisi na haraka.
Je wewe ni mtanzania unayeishi ughaibuni na ungependa kuweka akiba au kuwekeza nyumbani na kupata ukaribu na wapendwa wako kifedha? Akaunti ya Tanzanite ndio suluhisho lako. Akaunti hii ni maalumu kwa ajili ya watanzania wanaoishi nje ya nchi, inayowasaidia kuweka akiba, kuwekeza na kukidhi majukumu binafsi, kikazi au ya masomo kwa urahisi na haraka.
- Hakuna makato ya uendeshaji wa akaunti
- Akaunti inaweza kufunguliwa kwa sarafu nne: TZS, USD, GBP, na EURO
- Akaunti inaweza kufunguliwa kupitia App ya SimBanking
- Fursa ya Mikopo ya Nyumba (Mortgage); Ununuzi, Ujenzi, Ukarabati, Kumalizia nyuma na uthaminishaji (Equity release)
- Viwango vya riba shindani kwenye akaunti za muda maalum (Fixed Accounts)
- Bima ya KAVA ambayo ni BURE kwa mmiliki wa akauti na Mwenza/Wenza wake wa ndoa mpaka wake wanne
- Kadi za malipo na njia za kidijitali zitakazokuwezesha kutumia akaunti yako popote ulipo Duniani
- Utaunganishwa na Internet Banking na SimBanking zinazopatikana kwa masaa 27 siku saba za wiki
- Mameneja Uhusiano watakaokuhudumia masaa 24 siku 7 za wiki.
- Usimamizi wa Mali na Ushauri wa Uwekezaji.
Meneja Mahusiano maalumu kwa kila mteja anayeishi nje ya nchi
Gharama nafuu za kuendesha akaunti na kufanya miamala
Unaunganishwa na huduma za utumaji pesa kwa urahisi na haraka
Unapata Huduma ya KAVA Assurance Bure (Mteja binafsi na/au mwenza wake): Bima ya Maisha TSH Milioni 5, endapo kifo kitatokea, utalipiwa gharama za kusafisha mwili hadi TSH Milioni 15.
Unapata riba kulingana na akiba yako
Kupitia akaunti ya Tanzanite unaweza kupata mkopo wa Nyumba wa muda mrefu kwa masharti na gharama nafuu
Unapata kadi ya TemboCard Visa Gold inayokuwezesha kufanya miamala kwa urahisi duniani kote
Unapata huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi (Simbanking) pamoja na mtandao.
Akaunti ni kwa ajili watanzania waishio nje ya nchi wenye umri wa miaka 18 au zaidi
Nakala ya Pasipoti au Kitambulisho cha Taifa
Kibali cha kazi/makazi au Visa
Uthibitisho wa makazi mfano Bili ya maji au mkataba wa pango n.k.
Picha 2 za pasipoti saizi
--------------
Kwa mwanafunzi: Nakala iliyothibitishwa ya barua ya utambulisho au ya kujiunga na shule
Tuandikie kupitia barua pepe [email protected]
Maswali
Unaweza kupendezwa na
Jijenge
Mikopo ya Jijenge ni mikopo ya muda mrefu inayotolewa kwa wateja wa CRDB wenye malengo ya kujenga, kununua au equity release ya nyumba.
Bima ya KAVA
Bima ya KAVA ni huduma ya bima inayotolewa BURE kwa wateja wa CRDB wenye Akaunti binafsi.