Akaunti ya Yanga

Maelezo

Wewe ni mmoja wa mabingwa?

Mwananchi, ni muda muafaka wa kuwa shabiki au mwananchama wa faida kwa kuichangia timu yako kupitia benki ya CRDB.

Benki ya CRDB kwa kushirikiana na klabu ya Yanga wameingia makubaliano ya kukupatia kadi maalum ambayo itakutambulisha wewe kama shabiki pamoja na kukuwezesha kufanya miamala yote ya kibenki.

Una akaunti ya CRDB tayari?

Kama wewe ni Shabiki au Mwanachama wa Yanga na una akaunti ya CRDB basi hautatakiwa kufungua akaunti nyingine. Unachotakiwa kufanya ni 


  • Kufika tawini ukiwa na kitambulisho halali

  • Utajaza fomu ya kuomba kadi

  • Mwanachama atahitajika kulipa Tsh 24,000 kama ada ya mwaka.

  • Shabiki atahitajika kulipa Tsh 12,000 kama mchango wa klabu.


Hauna akaunti ya CRDB?

Kama wewe ni Shabiki au Mwanachama wa Yanga na hauna akaunti ya benki ya CRDB, basi utatakiwa kufungua akaunti ambayo itakuwezesha kuweka akiba, kufanya malipo mbalimbali yakiwemo ya ushabiki na huduma nyingine za kibenki.


Faida za kuwa na Kadi ya Yanga

  • Kukutambulisha kama mwanachama halali wa timu ya Yanga

  • Kufanya miamala kupitia ATM, CRDB Wakala, Machine za POS n.k

  • Mwanachama anapata bima ya Maisha hadi Tsh 2,000,000 pindi atakapopata ulemavu wa kudumu, kufariki au kufiwa na mwenza.


Kiasi cha kuanzia (Initial deposit)

Akaunti ya Yanga inafunguliwa kwa kiwango cha Tsh 2,000/= ambayo shabiki atatakiwa kulipia sambamba na gharama nyingine za kadi kama ilivyoainishwa hapo chini kulingana na aina ya kadi atakayoomba.

Kwa Mwanachama anatakiwa kuwa na:

  • Kitambulisho Kimojawapo (NIDA ID, Voters ID, Driver’s License, Zanzibar ID au Passport) 

  • Namba yake ya uanachama 

  • Ada ya uanachama ya shilingi 24,000/= kwa mwaka


Kwa Shabiki anatakiwa kuwa na;

  • Kitambulisho Kimojawapo (NIDA ID, Voters ID, Driver’s License, Zanzibar ID au Pasipoti) 

  • Ada ya shabiki shilingi 12,000/= (kwa mwaka) 


Gharama ya Kadi ya Yanga ni kiasi gani? 

  • Kuanzia tarehe 05/07/2023 mpaka 05/08/2023, Benki ya CRDB itatoa Kadi ya Yanga BURE lakini Mwanachama/Shabiki atatakiwa kulipa shilingi 24,000/= kama gharama ya uanachama 

  • Baada ya tarehe 05/08/2023 mteja atatakiwa kulipia 5,000/= kwa ajili ya kadi Pamoja na shilingi 24,000/= ya uanachana (Jumla Shilingi 29,000/=)

Unaweza kupendezwa na