Akaunti ya hundi

Maelezo

Rahisi, ya kuaminika, yenye unafuu

Tunafahamu una matarajio na ndoto zako, hivyo Akaunti yetu ya Hundi itakupa njia rahisi ya kushughulikia miamala ili kufanikisha ndoto na mipango yako. Akaunti ya Hundi ya Benki ya CRDB inakidhi mahitaji yako ya kila siku ya kibenki. Furahia urahisi wa kulipa kwa hundi na kuchukua pesa bila vikwazo, njia bora ya kukamilisha shughuli zako wakati wowote, mahali popote.

Sifa 5 bora za Akaunti yetu ya Hundi

  • Akaunti inaweza kufunguliwa na kuendeshwa kwa TZS, USD, EURO, GBP

  • Salio la chini kabisa la TZS 100,000, USD 100, GBP 100, au EURO 100.

  • Unaweza kutumia hundi kutoa na kuhamisha fedha

  • Mtia saini anapewa TemboCard Visa/MasterCard 

  • Unapata huduma ya overdraft (Ikiwa umekidhi masharti ya mkopo).

Sababu 4 za kufungua Akaunti ya Hundi

  • Unaweza kufanya miamala mtandaoni

  • Unapata huduma za SimBanking 

  • Una njia nyingi na rahisi za kufanya malipo yaani hundi, mtandaoni na SimBanking

  • Inaruhusu mtia saini zaidi ya mmoja.

Kufungua akaunti:

  • Uwe na umri wa miaka 18 na zaidi

  • Uwe kitambulisho halali (NIDA, Kitambulisho cha Mpiga Kura, Pasipoti, Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha Zanzibar)

  • Uwe na picha 2 za pasipoti

Unaweza kupendezwa na