ATM ya kuweka fedha

Maelezo

Badilisha hali yako ya utumiaji wa benki ukitumia Mashine za Kuweka Fedha za CRDB—zinazotoa huduma masaa 24/7 , usalama na matumizi yaliyorahisishwa kwa mtumiaji, yote yameundwa ili kufanya utunzaji wa fedha kwa haraka na ufanisi zaidi kwa wateja.

Mashine ya kuweka fedha ni mashine ya kiotomatiki inayowawezesha wateja wa CRDB kuweka fedha kwenye akaunti zao za benki bila kuhitaji mtoa huduma wa benki.

Inavyofanya kazi:

Utambuzi: Mteja aweke namba ya akaunti ya CRDB anayotaka kuweka pesa taslimu (Wakala na akaunti za shule zinakubaliwa pia).

Weka Fedha: Machine prompts users to insert cash. CRDB CDM accepts 5000 and 10,000 TZS denominations only and counts the total amount deposited. Mashine itakuelekeza kuweka pesa taslimu. CDM ya CRDB inakubali fedha za TZS 5000 na 10,000 pekee na kuhesabu jumla ya kiasi kilichowekwa.

Thibitisha: Baada ya kuweka pesa, mteja hupokea risiti na arifa ya SMS kuthibitisha muamala. CDM zinafaa kwa amana za haraka na mara nyingi zinaweza kutumika nje ya saa za kawaida za benki.

Urahisi
  • Skrini ya kugusa: Maelekezo mepesi ya jinsi ya kuweka fedha
  • Usaidizi wa Lugha nyingi: Hutoa chaguzi mbalimbali za lugha kwa wateja mbalimbali (Kiingereza na Kiswahili).
Uwezo wa kupokea fedha
  • Utambuzi wa fedha: Uwezo wa kupokea noti mbalimbali, kuzitambua na kuzihesabu kwa usahihi (5K & 10K)
  • Kupokea fedha nyingi: Uwezo wa kupokea na kutambua fedha mbalimbali kwa wakati mmoja.
Usalama wa Miamala
  • Teknologia ya kiusalama: Hulinda data ya mteja na maelezo ya muamala.
  • Uwepo wa kamera za CCTV & Faragha: CDM zetu zina kamera na chumba cha faragha ili kuzuia ulaghai na kuhakikisha usalama/faragha wakati wa muamala.

Uthibitisho wa fedha kuingia wa papo hapo


  • Risiti za Kidijitali:. Hutoa uthibitisho wa papo hapo wa muamala kupitia risiti iliyochapishwa na SMS kwenye simu ya mteja.
  • Masasisho ya Wakati Halisi: Husasisha salio la akaunti mara moja, ili kuruhusu watumiaji kuona amana zao zikionyeshwa mara moja.

Urahisi
  • Upatikanaji 24/7: Huruhusu wateja kuweka pesa wakati wowote, na hivyo kuondoa hitaji la kutembelea benki wakati wa saa za kazi..
  • Miamala ya Haraka: Huboresha mchakato wa kuweka pesa, kupunguza muda wa kusubiri ikilinganishwa na huduma za kawaida za malipo.
Matumizi rafiki
  • Matumizi yaliyo rahisishwa: Rahisi kutumiwa na mtu yoyote
  • Usaidizi wa Lugha nyingi: Hutoa chaguzi mbalimbali za lugha kwa wateja mbalimbali (Kiingereza na Kiswahili).
Usalama Ulioimarishwa
  • Usalama wa Miamala: Teknologia yenye kulinda data ya mteja na maelezo ya muamala.

Kuongezeka kwa Kuridhika kwa Wateja

  • Huduma ya haraka zaidi: Michakato ya haraka ya kuweka fedha huongeza uzoefu na kuridhika kwa wateja.
  • Ufanisi: Wateja wanaweza kukidh mahitaji yao ya benki kwa ufanisi zaidi, na hivyo kusababisha kuongezeka kwa uaminifu.
Environmental Benefits
  • Kupunguza Matumizi ya Karatasi: Huhimiza mazoea ya benki ya kidijitali na kupunguza utegemezi wa stakabadhi za karatasi na nyaraka.

Jina la Tawi
Mkoa
ARUSHA BRANCH
Arusha
BANANA BRANCH
Dar es salaam
BUNJU BRANCH
Dar es salaam
CHAMWINO BRANCH
Dodoma
GONGO LA MBOTO BRANCH
Dar es salaam
IRINGA BRANCH
Iringa
KAHAMA BRANCH
Shinyanga
LIVINGSTONE BRANCH
Mbeya
LUMUMBA BRANCH
Dar es salaam
MBAGALA BRANCH
Dar es salaam
MBEZI BEACH BRANCH
Dar es salaam
MBEZI LUIS BRANCH
Dar es salaam
MLIMANI CITY BRANCH
Dar es salaam
MOROGORO BRANCH
Morogoro
MOSHI BRANCH
Kilimanjaro
MTWARA BRANCH
Mtwara
NJOMBE BARNCH
Njombe
NYANZA BRANCH
Mwanza
SONGEA BRANCH
Ruvuma
TANDIKA BRANCH
Dar es salaam
TEGETA BRANCH
Dar es salaam
SINGIDA BRANCH
Singida

Maswali

Hakuna kikomo cha kuweka pesa, hata hivyo machine inapokea pesa katika kifungu ya noti 200 kwa muamala mmoja.

Ndio, Kabla ya kuthibitisha muamala, mteja anaweza kuamua kughairi muamala na kurejeshewa pesa taslimu..

Unaweza kupendezwa na