Bima ya Maisha ya Kikundi

Maelezo

Tunafurahi kukuletea huduma ya thamani kwenye akaunti yako ya kikundi. Bima yetu ya Maisha ya Kikundi inakulinda wewe na familia yako dhidi ya hatari zisizo na mpango. 

Faida hii ya ziada inajumuisha ulinzi dhidi ya majanga baada ya kifo, ulemavu wa kudumu na jumla, na faida za elimu kwa watoto wako. Kuweza kupata faida hii ya kipekee, kikundi chako kinahitaji kuwa na zaidi ya wanachama 10, na kila mwanachama lazima awe raia wa Tanzania kati ya umri wa miaka 21 na 75. Mbali na hayo, wanachama wanaweza kuchagua kuwalinda wazazi wao na wakwe ambapo kiwango cha juu cha umri ni miaka 90.


•⁠  ⁠Utulivu wa akili kwa wewe na familia yako

•⁠  ⁠⁠Ulinzi wa kifedha endapo kutatokea majanga yasiyotegemewa

•⁠  ⁠⁠Manufaa ya elimu kwa watoto wako

•⁠  ⁠⁠Ulinzi wa ziada kwa wazazi na wakwe

•⁠  ⁠⁠Inahusu kifo, ulemavu wa kudumu na wa jumla

•⁠  ⁠Kikundi chenu lazima kiwe na angalau wanachama 10

•⁠  ⁠⁠Kila mwanachama lazima awe Mtanzania mwenye umri kati ya miaka 21 hadi 75

•⁠  ⁠⁠Wanachama wanaweza kuchagua kuwalinda wazazi wao na wakwe, kwa umri usiozidi miaka 90

•⁠  ⁠⁠Wasilisha barua ya utambulisho kutoka kwa kiongozi wa kikundi

•⁠  ⁠⁠Wasilisha nakala za vitambulisho kama vile NIDA, Kadi ya Mpiga Kura, Pasipoti, au Leseni ya Udereva

•⁠  ⁠⁠Fomu ya maombi iliyosainiwa na orodha ya wanachama wa kikundi wanaohitaji bima

Unaweza kupendezwa na