Akaunti ya Simba
Maelezo
Wewe ni shabiki wa faida?
Wewe ni shabiki kindakindaki wa mnyama? Ni muda muafaka wa kuwa shabiki wa faida kwa kuichangia timu yako kupitia benki ya CRDB.
Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Simba Sports Club wameingia makubaliano ya kukupatia kadi maalum ambayo itakutambulisha wewe kama shabiki pamoja na kukuwezesha kufanya miamala yote ya kibenki.
Una akaunti ya CRDB?
Kama wewe ni shabiki wa Simba na una akaunti ya CRDB basi hautatakiwa kufungua akaunti nyingine. Unachotakiwa kufanya ni kuomba kadi ya Simba moja kwa moja kupitia SimBanking au tawi lolote la benki ya CRDB.
Je, hauna akaunti ya CRDB?
Kama wewe ni shabiki wa Simba na hauna akaunti ya benki ya CRDB, basi utatakiwa kufungua akaunti maalum ya Simba ambayo itakuwezesha kuweka akiba, kufanya malipo mbalimbali yakiwemo ya ushabiki na huduma nyingine za kibenki.

Kiasi cha kuanzia (Initial deposit)
Akaunti ya Simba inafunguliwa kwa kianzio cha Tsh 2,000/= sambamba na gharama nyingine za kadi kama iliyoainishwa hapa chini kulingana na aina ya kadi utakayoomba.
Aina za kadi
Shabiki wa Simba anaweza kuomba moja wapo ya kadi zifuatazo mara tu atakapofungua akaunti ya Simba kupitia benki ya CRDB au kama tayari ana akaunti ya CRDB.
Kadi ya Watoto “Simba Cub Card”
Kadi ya Kawaida kwa Wanawake na Wanaume “Simba Classic Card”
Kadi ya VIP “Simba Platinum Card”
Simba Cubs Card
Ada yake ni Tsh 12,000
Inakutambulisha kama mtoto shabiki wa Simba
Unaweza kufanya miamala kupitia POS, ATM, CRDB Wakala n.k
Unaweza kutoa hadi Tsh 2,000,000 kwa siku kwenye ATM lakini pia utaweza kulipia hadi tsh 10,000,000 kwenye POS na mtandaoni
Simba Classic Card
Ada yake ni Tsh 12,000
Inakupa bima ya Maisha ya hadi Tsh 2,000,000 endapo utapata ulemavu wa kudumu, kufariki au kufiwa na mwenza.
Inakutambulisha kama shabiki halali wa Simba
Unaweza kufanya miamala kupitia POS, ATM, CRDB Wakala n.k
Unaweza kutoa hadi Tsh 2,000,000 kwa siku kwenye ATM lakini pia utaweza kulipia hadi tsh 10,000,000 kwenye POS na mtandaoni
Simba Platinum Card
Ada yake ni Tsh 38,400/=
Inakupa bima ya Maisha ya hadi Tsh 10,000,000 endapo utapata ulemavu wa kudumu, kufariki au kufiwa na mwenza.
Unapata kipaumbele kwenye matukio ya klabu ya Simba
Unapata huduma maalum kwenye matawi ya CRDB (Premier Lounges)
Inakutambulisha kama shabiki halali wa Simba
Unaweza kufanya miamala kupitia POS, ATM, CRDB Wakala n.k
Unaweza kutoa hadi Tsh 15,000,000 kwa siku kwenye ATM lakini pia utaweza kulipia hadi tsh 30,000,000 kwenye POS na mtandaoni
Upatikanaji wa Kadi
Kama wewe ni shabiki wa Simba mwenye akaunti ya CRDB;
- Tembelea tawi la CRDB ukiwa na kitambulisho kinachotambulika na serikali.
- Utajaza fomu ya kuomba kadi unayohitaji.
Kama wewe ni shabiki wa Simba ambaye hauna akaunti ya CRDB;
Fika tawini ukiwa na kitambulisho kimojawapo (NIDA, Mpira Kura, Udereva, Zanzibar, au Pasi ya kusafiria.
Utafunguliwa akaunti ya Simba na kujaza fomu ya kuomba kadi ya Simba
Unaweza kupendezwa na
Akaunti ya hundi
Akaunti ya hundi ya benki ya CRDB ni akaunti inayotumia njia rahisi mbalimbali za miamala kwa ajili ya kutimiza malengo yako ya kibenki
Akaunti ya Malkia
Akaunti ya Malkia ni akaunti ya wanawake iliyo na lengo la kufanikisha mipango yako ya kuweka akiba kwa ajili yako.
Akaunti ya Akiba
Ukiwa na akaunti ya akiba, utaweza kuweka akiba itakayokusaidia kwa ajili ya mahitaji yako ya baadae
Akaunti ya Junior Jumbo
Akaunti hii ni mahsusi kwa wazazi au walezi kuweza kuwawekea akiba watoto wao.
Akaunti ya Scholar
Akaunti ya akiba iliyoundwa kwa wanafunzi kuwawezesha kuendesha mahitaji yao ya kifedha na kujikimu wakiwa chuo kikuu au shuleni.
Akaunti ya Salary
Hii ni Akaunti ya akiba inayowezesha malipo yako ya mshahara kutoka kwa mwajiri wako ambaye ni kampuni au taasisi na ni mteja wa CRDB Bank.
Akaunti ya Teen
Akaunti maalum inayofunguliwa na kuendeshwa na mzazi/mlezi kwa ajili ya kijana wake mwenye umri kuanzia miaka 13 hadi 17
Niamoja
Akaunti maalum kwa ajili ya vikundi inayorahisisha ukusanyaji na usimamizi wa michango ya kikundi. Pia kikundi kinakuwa na uhakika juu ya usalama wa michango ya kikundi. Vikundi vya Nia Moja ni kama; • VICOBA, Vikundi vya kifamilia, vikundi vya kwenye mit
Akaunti ya Pensheni
Akaunti hii ya akiba ni maalum kwa ajili ya wastaafu inakuwezesha kupokea malipo ya pensheni ya mkupuo na ya kila mwezi na mapato mengine pia
Akaunti ya Yanga
Fungua akaunti maalum ya Yanga ambayo itakuwezesha kuweka akiba, kufanya malipo mbalimbali yakiwemo ya ushabiki na huduma nyingine za kibenki.