Mkopo wa “Overdraft” (Jinasue Overdraft)
Maelezo
Jinasue ni huduma ya mkopo wa kidijitali wa haraka na rahisi unaomuwezesha mteja kuomba na kurejesha mikopo moja kwa moja kupitia simu yake ya mkononi. Huduma hii inapatikana muda wote (24/7) kwa kutumia simu ya mkononi kupitia aplikesheni ya SimBanking au USSD (kwa kupiga *150*03#).
Hii ni huduma ya mkopo inayoongeza salio kwenye akaunti ya mteja pale ambapo salio lililopo halitoshi kukamilisha muamala. Hii inamwezesha mteja kufanya miamala hata akiwa hana fedha ya kutosha.
Jinasue ni huduma ya mkopo wa kidijitali wa haraka na rahisi unaomuwezesha mteja kuomba na kurejesha mikopo moja kwa moja kupitia simu yake ya mkononi. Huduma hii inapatikana muda wote (24/7) kwa kutumia simu ya mkononi kupitia aplikesheni ya SimBanking au USSD (kwa kupiga *150*03#).
Hii ni huduma ya mkopo inayoongeza salio kwenye akaunti ya mteja pale ambapo salio lililopo halitoshi kukamilisha muamala. Hii inamwezesha mteja kufanya miamala hata akiwa hana fedha ya kutosha.
Kiasi cha Mkopo: Hadi shilingi 1,000,000.
Muda wa Kulipa: Hulipwa mara tu mteja anapoweka fedha kwenye akaunti au ndani ya siku 30, kutegemea kipi kitaanza kwanza.
Riba nafuu na shindani.
Mkopo unapatikana kupitia SimBanking App au USSD.
Mteja anaweza kutumia huduma hii mara nyingi atakavyo ilimradi tu hajavuka kikomo kilichoidhinishwa.
Fedha inatolewa papo hapo wakati wa kufanya muamala.
Matumizi: Inaweza kutumika kukamilisha miamala muhimu kama vile:
Kuhamisha fedha Kwenda akaunti za CRDB, benki nyingine au mitandao ya simu.
Malipo ya huduma kama LUKU, maji, TV, n.k.
Malipo ya tiketi za ndege, bima, ada za shule, na mengineyo mengi
Mteja lazima awe na akaunti hai ya CRDB iliyounganishwa kwenye SimBanking.
Wafanyakazi: Wanapata mkopo hadi 50% ya mshahara wa mwezi baada ya makato
Wateja Wengine: Kiwango kitategemea wingi wa miamala wanayofanya kupitia akaunti zao.
Maswali
Jinasue OD ni njia rahisi ya kukamilisha muamala wako wakati hauna pesa za kutosha kwenye akaunti yako. Inakuruhusu kukopa kiasi kinachohitajika ili kufanikisha ununuzi, malipo, au uhamisho wa fedha.
Unapoanzisha muamala na hauna pesa za kutosha kwenye akaunti yako, Jinasue itakupa chaguo la mkopo wa Jinasue OD. Ukikubali, kiasi kinachohitajika kitawekwa mara moja kwenye akaunti yako, na hivyo kuweza kukamilisha muamala bila usumbufu.
Vigezo vitategemea historia ya matumizi ya akaunti yako, ikiwa ni Pamoja na historia ya miamala ya akaunti yako na uaminifu wako wa kulipa mikopo.
Kiwango cha mkopo kinategemea mambo mbalimbali, ikiwemo historia ya akaunti yako, uaminifu wa mkopo, na sera za benki. Ujumbe utaonyesha kiwango unachoweza kupata unapochagua Jinasue OD.
Kiwango cha juu cha mkopo ni TZS 1,000,000.
Kuna ada ya mara moja ya 8% inayotozwa kwenye kiasi cha mkopo.
Kiasi cha mkopo, pamoja na ada na riba yoyote inayotumika, kitakatwa moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako baada ya kuweka amana inayofuata. Huhitaji kuchukua hatua yoyote ya ziada kulipa mkopo. Hata hivyo, mkopo unapaswa kulipwa kikamilifu ndani ya siku 30.
Muda wa mkopo ni mwezi mmoja, yaani, siku 30. Unaweza kulipa mkopo wako ndani ya mwezi kupitia amana kadhaa. Ikiwa hutalipa mkopo ndani ya siku thelathini, ada na riba za ziada zinaweza kutumika. Ni muhimu kusimamia fedha zako kwa uwajibikaji na kuhakikisha una pesa za kutosha kulipa mkopo.
Mkopo unapatikana wakati wa malipo au kuhamisha pesa kupitia simbanking, wakati akaunti yako ikiwa haina salio la kutosha.
Endapo unafanya muamala na akaunti yako haina pesa za kutosha, fuata maelekezo yatakayokuongoza hatua kwa hatua kwa hatua kuomba na kupokea mkopo wa Jinasue OD kukamilisha muamala wako.
Unaweza kupendezwa na
Mkopo wa Wafanyakazi
Pata mkopo wa Wafanyakazi hadi TZS Milioni 100 ndani ya masaa 24 na ‘Jiachie Utakavyo‘ na kiwango cha riba nafuu hadi 14% na muda wa marejesho hadi miaka 7.
Mkopo wa Jijenge
Mkopo wa muda mrefu unaotolewa kwa wateja na wateja watarajiwa wa benki ya CRDB kwa ajili ya Ujenzi, Kununua/Kukarabati nyumba za Kupanga.
Mkopo wa Boom Advance
Boom Advance ni mkopo wa muda mfupi unaokusudiwa kutoa suluhisho la kifedha la muda mfupi kwa wanafunzi kabla ya kupokea posho za HESLB.
Mkopo wa Salary Advance
Mkopo wetu wa Salary Advance ni njia isiyo na gharama kubwa ya kupata mkopo wa papo hapo hadi 50% ya mshahara wako kupitia SimBanking.
Mkopo wa Fedha Taslimu (Jinasue Cash Loan)
Huu ni mkopo wa muda mfupi unaotolewa moja kwa moja kwenye akaunti ya mteja ya CRDB ili kusaidia katika matumizi ya dharura au ya binafsi.