Nini Kipya?

Maswali

Taratibu za kufatilia gawio ni kama  kama ifatavyo;

  • Mwanahisa ataandika barua kwa katibu kudai gawio ambalo hajalipwa.
  • Atawasilisha barua hiyo tawi lolote la benki ya CRDB lililo karibu nae
  • Atajaza fomu ya kumbukumbu za mwanahisa ambayo ataambatisha nakala ya cheti cha hisa na kitambulisho chake cha Utaifa/kupigia kura/hati ya kusafiria/ leseni ya udereva na kuiacha tawini na kutumwa kwa  Katibu.

Mwanahisa anaweza kuwasiliana na ofisi ya hisa kupitia anuani ifuatayo: 

Katibu CRDB Bank Plc

Office Accommodation Scheme- Mtaa wa Azikiwe, Ghorofa ya 4 

S. L. P. 268 Dar-es-Salaam

Simu:  022 – 2114237, 255 753 260 176 – Fax na. 022 – 2131005

Barua pepe: [email protected], [email protected] au [email protected] 

Iwapo mwanahisa amepoteza cheti  chake cha hisa, anashauriwa kutoa taarifa Polisi ili apatiwe fomu ya polisi ya upotevu wa cheti cha hisa (Police report) kisha awasilishe tawi lolote la benki ya CRDB lililo karibu naye ili kujaza na kuleta nyaraka zifuatazo:

  • Barua (Application letter) 
  • Jaza fomu ya Kubadili taarifa kwenye cheti cha hisa (CDS Amendment form) 
  • Jaza fomu ya Upotevu wa cheti cha hisa (Replacement form) 
  • Taarifa ya Polisi ya upotevu wa Cheti cha Hisa (Police Loss Report) 
  • Nakala ya Kitambulisho cha Mwombaji.
  • Risiti ya Benki ya malipo TZS 2,000/= (kwenye Akaunti no. 0150305954000) ikiwa ni gharama ya kutengeneza cheti kipya na Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Baada ya mwanahisa kufariki, familia inatakiwa kukaa kikao na kumteua msimamizi wa mirathi ambaye anatakiwa kuthibitishwa na mahakama, msimamizi wa mirathi anatakiwa afuate utaratibu wa mirathi ya marehemu mahakamani kwa mujibu wa sheria. Baada ya taratibu zote kukamilika, msimamizi wa mirathi apeleke vielelezo vifuatavyo katika tawi lolote la benki ya CRDB lililo karibu naye au kwa Katibu wa Benki (Company Secretary):

  • Barua ya msimamizi wa mirathi (Application letter) 
  • Barua ya mahakama ya uteuzi wa Msimamizi wa mirathi (FORM No. IV) 
  • Jaza fomu ya Kubadili taarifa kwenye Cheti cha Hisa (CDS Amendment form) 
  • Nakala ya Cheti cha kifo cha marehemu 
  • Muhtasari wa Kikao cha ndugu (Minutes)
  • Nakala ya Kitambulisho cha msimamizi/Mrithi 
  • Risiti ya Benki ya malipo TZS 2,000/= (Akaunti no. 0150305954000) ikiwa ni gharama ya kutengeneza cheti kipya na Soko la Hisa la Dar es Salaam.
  • Nakala ya Cheti cha kuzaliwa cha msimamizi wa mirathi/ Kitambulisho cha Taifa
  • Nakala ya cheti cha ndoa cha msimamizi wa mirathi
  • Stakabadhi /Cheti Halisi cha Hisa (Original CDS Receipt)

Iwapo msimamizi wa mirathi hatakuwa na cheti cha hisa, itabidi ajaze fomu ya upotevu wa cheti cha hisa (DSE Replacement form) na kupata taarifa ya Polisi ya upotevu wa stakabadhi ya hisa.

Njia nyingine ni kupitia kwa mojawapo wa wakala wa Soko la Hisa na Mitaji la Dar es Salaam (Licensed Dealing Members of DSE).

Mwanahisa anaweza kubadilisha taarifa zake za hisa kwa kufanya yafuatayo:

  • Barua (Application letter)  
  • Cheti Halisi cha Hisa (Original CDS Receipt) au Nakala ya Cheti cha Hisa 
  • Risiti ya Benki ya malipo ya TZS 2,000/= (kwenye Akaunti no. 0150305954000)
  • Fomu ya Kubadili taarifa kwenye CDS (CDS Amendment form) 
  • Nakala ya kitambulisho cha Taifa/Kura/ Hati ya kusafiria (Passport)

Sheria hairuhusu Mwanahisa kukopa kwa dhamana ya Hisa zake katika benki/kampuni hiyo hiyo anayomiliki hisa, kufanya hivyo ni sawa na mtu kujikopa mwenyewe hivyo kupunguza mtaji. Hata hivyo Wanahisa wanaweza kuomba na kupata mikopo kutoka Benki kwa taratibu nyingine za kawaida kama wateja wengine. Vile vile wanaweza kukopa kupitia benki nyingine kwa kutumia hisa zao za benki ya CRDB kama dhamana ya mkopo.

Ndiyo unaweza. 

Kuna njia mbili mwanahisa anazoweza kutumia. Njia ya kwanza ni kwenda moja kwa moja kwa madalali wa soko la hisa ambao watakupa ushauri juu ya kuuza au kununua hisa na kufanya taratibu za kununua au kuuza hisa. Njia ya pili ni kupitia Benki ya CRDB kama Wakala wa dalali wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (Solomon Stockbrokers) kupitia matawi yote ya CRDB.

Benki ya CRDB kama wakala wa Solomon Stockbrokers inashiriki katika zoezi zima la kuuza na kununua hisa, kwa kuzingatia vigezo vyote vilivyowekwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam na Mamlaka ya Hisa na Mitaji. 

Katika kufanikisha wajibu wa uwakala Benki inatarajia kwamba mwekezaji anafanya maamuzi sahihi, na upembuzi wa kina, ikiwa ni pamoja na kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kuwekeza kwenye hisa. 

Uuzaji wa Hisa

Hata hivyo, Benki ya CRDB inatoa fursa ya kupatiwa mawasiliano ya washauri endapo utahitaji kufanya mawasiliano nao. Matawi yote ya Benki ya CRDB yanatoa huduma ya kuuza/kununua hisa.

Hatua hizi zitafuatwa na mwekezaji wakati wa kuweka maombi ya kuuza hisa:

  • Atapewa takwimu zinazohusu bei za hisa, hisa zinazouzwa, hisa zinazonunuliwa, na idadi ya hisa zilizouzika;
  • Atajaza fomu maalum za uuzaji wa hisa na ile ya taarifa muhimu zinazomuhusu mwekezaji;
  • Atatakiwa kuacha Stakabadhi ya hisa anazouza (DSE Depository receipt);
  • Afisa anayehusika atakagua fomu hizo kwa umakini kabla ya kuzifanyia kazi husika;
  • Ni vema kuacha mawasiliano yaliyo rahisi ikiwemo namba ya simu ya mkononi ili kupata taarifa mrejesho kwa haraka.

Benki kama wakala inapaswa kubaini uhalali wa umiliki wa hisa, mwekezaji atatakiwa pia kutoa vielelezo vingine kama  pasi ya kusafiria, kitambulisho cha kazi kilichotolewa na mwajiri anayefahamika na kitambukisho cha mpiga kura.

Wawekezaji watapewa mawasiliano ya moja kwa moja ya dalali, yaani SOLOMON Stockbrokers, ili waweze fuatilia kwa karibu mwenendo wa maombi yao ya hisa, na ikiwezekana kubadilisha maagizo ya awali pale inapobidi. Hii itasaidia kwa mwekezaji kufanya maamuzi ya haraka yaendanayo na kasi ya soko pale anapoona mabadiliko katika soko la hisa. 

Ununuzi wa Hisa

Hatua hizi zitafuatwa na mwekezaji wakati wa kuweka maombi ya kununua hisa:

  • Atapewa takwimu zinazohusu bei za hisa, hisa zinazouzwa, hisa zinazonunuliwa, na idadi ya hisa zilizouzika.
  • Atatakiwa kujaza fomu ya manunuzi ya hisa na ile ya taarifa muhimu zinazomhusu mwekezaji;
  • Ataweka pesa (Deposit) kwenye akaunti maalum ya dalali iliyopo katika benki ya CRDB. 
  • Atapewa stakabadhi ya malipo kama ushahidi wa malipo, ambayo atatakiwa kuionesha kwenye tawi wakati wa kupokea Stakabadhi ya Umiliki wa  Hisa    (DSE Depository Receipt).
  • Malipo yafanywe kwa pesa taslimu, hundi au ama kuhamisha pesa endapo akaunti inayolipa ipo kwenye tawi lolote la Benki ya CRDB.
  • Malipo kwa hundi hayatakiwi kuzidi kiasi cha shillingi milioni 10 kama taratibu za Benki Kuu zinavyohitaji, ama vinginevyo malipo yafanye kwa njia ya TISS (Tanzania Interbank

Ndio, mwanahisa anaruhusiwa kuhamisha hisa zake kwa ndugu zake wa karibu ambao ni baba,mama,mke,mume na mtoto kwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo katika tawi lolote la benki ya CRDB au kwa katibu wa benki.

  • Barua (Application letter)
  • Cheti Halisi cha Hisa (Original CDS Receipt) 
  • Risiti ya Benki ya malipo ya TZS 2,000/= (kwenye Akaunti no. 0150305954000)
  • Fomu ya Kubadili taarifa kwenye CDS (CDS Amendment form) 
  • Jaza fomu ya kuhamisha hisa (Private Transfer Form)
  • Kiapo kutoka kwa mwanasheria (Power of Attorney)
  • Cheti za kuzaliwa cha mtoto
  • Cheti cha ndoa
  • Nakala ya vitambulisho vya Taifa/Kura/ Hati ya kusafiria (Passport)Settlement System).

Kwa kawaida kampuni inapotangaza tarehe ya Gawio (mara nyingi kuchukua siku zaidi ya 14 au zaidi) hisa zitaanzwa kuuzwa na gawio pamoja na gawio liliotangazwa ndani yake (Cum dividend). Hivyo basi Mwanahisa yeyote atakaye uza hisa zake katika kipindi hiki atapoteza stahili yake ya gawio na hivyo hata pokea gawio, na Mwanahisa atakayenunua Hisa kipindi hiki atakuwa amepata stahili ya kupokea gawio hivyo ndiye atakayepata gawio.

Endapo Mwanahisa atanunua hisa baada ya tarehe ambayo Kampuni imefunga kipindi cha gawio yani mihamala bila gawio (Ex-dividend), mwanahisa huyo atanunua hisa bila gawio kwa kipindi chote mpaka kampuni itakapotangaza tena  tarehe ya gawio au kwa mwaka mwingine, kwa makampuni yanayotoa gawio mara moja kwa mwaka.Vivyo hivyo Mwanahisa atakayeuza hisa zake katika kipindi hiki, bado atastahili kupata gawio lake, pamoja atakuwa ameuza hisa zake.

Hivyo basi vipindi hivi ni muhimu sana kuzingatia, ili kuepusha hatari ya kuuza hisa huku ukitegemea gawio, wakati kipindi ulicho uza ni kipindi ambacho anayenunua ndiye gawio litaenda kwake, na endapo utauza kipindi hiki ni vizuri kupata ushauri wa wataalamu ambapo mara nyingi bei ya hisa ya kipindi cha cum dividend inatakiwa iwe juu kiasi kulingana na gawio litakalotolewa. Hivyo hata ukiuza kipindi hichi utazingatia bei itakayofidia kuachia gawio tajwa.