Rais Samia aipongeza CRDB kwa uwekezaji wake wa kijamii

By: | Blog | Septemba 10, 2021 04:56

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amepongeza jitihada zinazofanywa na Benki ya CRDB katika kuchangia maendeleo katika jamii.

Rais Samia ametoa pongezi hizo wakati wa kilele cha Tamasha la Kizimkazi alipokuwa akikabidhiwa miradi ya nyumba za madaktari na ofisi za shehia Kizimkazi Dimbani zilizojengwa kwa udhamini wa Benki hiyo.

Akipokea miradi hiyo iliyo gharimu kiasi cha shilingi milioni 300, Rais Samia alisema Serikali inajivunia ushirikiano wa kimaendeleo baina yake na Benki ya CRDB.

Aliongeza kuwa Benki hiyo imekuwa mfano mzuri wa ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya umma (PPP) kwa kufikia malengo yaliyowekwa katika Dira ya Maendeleo ya 2025. “Suala la kuijenga nchi yetu ni wajibu wa kila mmoja wetu na si la serikali peke yake, niwapongeze Benki ya CRDB kwa kujitoa kwenu kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Leo hii mmetutoa kimasomaso kwa kutusaidia kuimarisha sekta ya afya na kuhakikisha wananchi wa Kizimkazi Dimbani wanapata huduma bora za kijamii, ama hakika hii ni Benki ya kiza-lendo,” alisema Rais Samia.


Aidha, Rais Samia alisifu mafanikio ya Tamasha la Kizimkazi kwa mwaka huu 2021 ambalo lililenga katika kuhamasisha jamii kudumi-sha utamaduni na kuongeza ujumuishaji wa kiuchumi kwa wananchi kwa kuonyesha fursa mbalimbali zitokanazo na tamaduni za Kitanzania.

Tamasha hilo lilihusisha mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 500 juu ya ubunifu wa bidhaa za asili, elimu ya fedha na uendeshaji biashara, pamoja na michezo mbalim-bali ya asili.Pia alieleza kwamba wakati umewadia kwa Watanzania kuacha utamaduni wa kigeni na kujivunia utamaduni wetu. Alitoa rai kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa na mikakati mbalimbali itakayosaidia kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania.

Rais Samia alisema jamii pia ina wajibu wa kushiriki kikamilifu katika matamasha ya utamaduni ili kusaidia ukuzaji na uendelezaji wa mfumo wa utamaduni na sanaa katika jamii ya Kitan-zania. “Benki ya CRDB imetuon-yesha kwa mfano kuwa tukiwekeza katika utamaduni wetu tutafungua fursa nyingi za kiuchumi kwa kutengeneza soko kwa bidhaa zetu za asili na Sanaa yetu.

Kupitia Tamasha hili la Kizimkazi niiombe Wizara iweke mikakati ya kuanzisha matamasha ya utamaduni katika kila kanda hii itasaidia kukuza tamaduni za maeneo mbalimbali na kuchochea utalii,” alisisitiza Rais Samia.

Mwananchi