CRDB Wakala

Maelezo

Benki ya CRDB kupitia mtandao wa CRDB Wakala imetoa fursa ya ajira kwa zaidi ya watanzania 45,000 waliojitolea kutoa huduma za kibenki kwa niaba ya Benki ya CRDB. Tunakaribisha mfanyabiashara yeyote mwanye uwezo ajiunge na jitihada zetu za kutoa huduma za benki kwa urahisi kila mahali na kupata faida kubwa zaidi.

 • Kutanua wigo wa biashara kwa kufanya kazi na Taasisi ya kifedha inayoongoza nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla
 • Pata kamisheni ya kuvutia kwa kutoa huduma kwa wateja wakubwa nchini kote
 • Ongeza mauzo katika biashara yako ya awali kwa kutembelewa na wateja wengi wa CRDB
 • Ongeza ufanisi kwenye biashara yako kwenye usimamizi wa fedha kwani utakuwa unahudumia wateja wa CRDB wanaotoa fedha hivyo kupunguza hatari ya kukaa na fedha
 • Jenga uwezo kupitia mafunzo ya bure katika maeneo ya ujasiriamali, huduma za kibenki, na kupambana na udanganyifu wa kifedha.

 • Lazima uwe mfanyabiashara binafsi au kampuni
 • Ni lazima uwe na biashara inayoendelea, inayoendeshwa kihalali na uwe na leseni ya biashara
 • Uwe unafanya kazi katika eneo la biashara la kudumu lenye miundombinu inayofaa, uwezo wa kifedha na rasilimali watu ili kuweza kutoa huduma kwa ufanisi na usalama.
 • Mtu/Biashara lazima isiwe na rekodi mbaya ya madeni kwenye benki au taasisi yoyote ya kifedha kwa muda wote wa makubaliano ya uwakala
 • Mtu/Biashara haitakiwi kuendesha huduma ya Benki kama shughuli yake pekee na lazima uwe na kitambulisho cha NIDA
 • Mtaji wa chini kabisa ni Tsh Milioni 2 na ada ya maombi ya uwakala ni Tsh 350,000 ambayo haiwezi kurejeshwa mara wakala atakapoidhinishwa na kusaini makubaliano.

Unaweza kupendezwa na