Benki Mtandaoni

Maelezo

CRDB benki ya mtandao(CRDB internet banking) ni njia ya haraka kwa usimamizi wa kifedha mkondoni, ambapo unaweza kupata habari ya akaunti yako kwa urahisi na kufanya miamala mbalimbali kwa usalama na kwa urahisi. Internet banking inakusaidia kufikia akaunti yako binafsi au ya biashara saa 24 popote ulipo.

  • Unaweza kuhamisha hela kwenye akaunti ya benki kwenda kwenye mitandao ya simu (M-PESA, TIGOPESA, Airtel Money na Halopesa).
  • Malipo ya mkupuo kwenda kwenye mtandao wa simu (M-PESA, TIGOPESA, Airtel Money na Halopesa).
  • Malipo mkupuo wa muda wa maongezi wa simu ya mkononi.
  • Malipo ya mkupuo kwa akaunti Benki ya CRDB, akaunti ya benki nyingine (EFT na TISS).
  • Malipo ya kimataifa kupitia SWIFT.
  • Malipo ya ankara mbalimbali (DSTV, Precision Air, Airtime, Azam TV, TRA, LUKU) nk.
  • Malipo ya serikali kupitia GEPG.
  • Uhamishaji wa pesa za kigeni (yaani TZS TO FX, FX TO FX, FX TO TZS), uhamisho huu wote unaweza kufanywa kwa kutumia kiwango cha bodi kilichoidhinishwa au kiwango cha mazungumzo (Kiwango maalum).
  • Kuangalia salio
  • Taarifa fupi na taarifa kamili

  • Kukupatia uwezo wa kudhibiti akaunti yako 24/7
  • Huokoa muda na kukupa huduma nzuri.
  • Inahakikisha Usiri wako na Usalama
  • Usalama wa akaunti ya mteja unalindwa na ngazi mbili kwa kutumia jina la mtumiaji na Nenosiri pamoja na OTP inayopatikana kwa SMS, application ama kifaa maalum.
  • Inaruhusu kuwa na watumiaji wengi wenye viwango mbalimbali vya matumizi kwa watumiaji wa kampuni.
  • Inaruhusu uwepo wa viwango tofauti vya kufanya/kuhakiki miamala kwa watumiaji wa kampuni.

  • Tafadhali tembelea tawi lililo karibu nawe ukiwa na kitambulisho chako (NIDA, Kadi ya Mpiga Kura, Pasipoti au Leseni ya udereva) ikiwa uko ndani ya Tanzania.
  • Ikiwa uko nje ya nchi tafadhali tutumie barua pepe kupitia [email protected] au [email protected]

Unaweza kupendezwa na