Akaunti ya Simba

Maelezo

Wewe ni shabiki wa faida?


Wewe ni shabiki kindakindaki wa mnyama? Ni muda muafaka wa kuwa shabiki wa faida kwa kuichangia timu yako kupitia benki ya CRDB.


Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Simba Sports Club wameingia makubaliano ya kukupatia kadi maalum ambayo itakutambulisha wewe kama shabiki pamoja na kukuwezesha kufanya miamala yote ya kibenki.


Una akaunti ya CRDB?

Kama wewe ni shabiki wa Simba na una akaunti ya CRDB basi hautatakiwa kufungua akaunti nyingine. Unachotakiwa kufanya ni kuomba kadi ya Simba moja kwa moja kupitia SimBanking au tawi lolote la benki ya CRDB.


Je, hauna akaunti ya CRDB?

Kama wewe ni shabiki wa Simba na hauna akaunti ya benki ya CRDB, basi utatakiwa kufungua akaunti maalum ya Simba ambayo itakuwezesha kuweka akiba, kufanya malipo mbalimbali yakiwemo ya ushabiki na huduma nyingine za kibenki.

Kiasi cha kuanzia (Initial deposit)

Akaunti ya Simba inafunguliwa kwa kianzio cha Tsh 2,000/= sambamba na gharama nyingine za kadi kama iliyoainishwa hapa chini kulingana na aina ya kadi utakayoomba.


Aina za kadi

Shabiki wa Simba anaweza kuomba moja wapo ya kadi zifuatazo mara tu atakapofungua akaunti ya Simba kupitia benki ya CRDB au kama tayari ana akaunti ya CRDB.


  1. Kadi ya Watoto “Simba Cub Card”

  2. Kadi ya Kawaida  kwa Wanawake na Wanaume “Simba Classic Card”

  3. Kadi ya  VIP “Simba Platinum Card”

Simba Cubs Card

  • Ada yake ni Tsh 12,000

  • Inakutambulisha kama mtoto shabiki wa Simba

  • Unaweza kufanya miamala kupitia POS, ATM, CRDB Wakala n.k

  • Unaweza kutoa hadi Tsh 2,000,000 kwa siku kwenye ATM lakini pia utaweza kulipia hadi tsh 10,000,000 kwenye POS na mtandaoni


Simba Classic Card

  • Ada yake ni Tsh 12,000

  • Inakupa bima ya Maisha ya hadi Tsh 2,000,000 endapo utapata ulemavu wa kudumu, kufariki au kufiwa na mwenza.

  • Inakutambulisha kama shabiki halali wa Simba

  • Unaweza kufanya miamala kupitia POS, ATM, CRDB Wakala n.k

  • Unaweza kutoa hadi Tsh 2,000,000 kwa siku kwenye ATM lakini pia utaweza kulipia hadi tsh 10,000,000 kwenye POS na mtandaoni


Simba Platinum Card

  • Ada yake ni Tsh 38,400/=

  • Inakupa bima ya Maisha ya hadi Tsh 10,000,000 endapo utapata ulemavu wa kudumu, kufariki au kufiwa na mwenza.

  • Unapata kipaumbele kwenye matukio ya klabu ya Simba

  • Unapata huduma maalum kwenye matawi ya CRDB (Premier Lounges)

  • Inakutambulisha kama shabiki halali wa Simba

  • Unaweza kufanya miamala kupitia POS, ATM, CRDB Wakala n.k

  • Unaweza kutoa hadi Tsh 15,000,000 kwa siku kwenye ATM lakini pia utaweza kulipia hadi tsh 30,000,000 kwenye POS na mtandaoni

Upatikanaji wa Kadi

Kama wewe ni shabiki wa Simba mwenye akaunti ya CRDB;

  • Tembelea tawi la CRDB ukiwa na kitambulisho kinachotambulika na serikali.
  • Utajaza fomu ya kuomba kadi unayohitaji.


Kama wewe ni shabiki wa Simba ambaye hauna akaunti ya CRDB;

  • Fika tawini ukiwa na kitambulisho kimojawapo (NIDA, Mpira Kura, Udereva, Zanzibar, au Pasi ya kusafiria.

  • Utafunguliwa akaunti ya Simba na kujaza fomu ya kuomba kadi ya Simba

Unaweza kupendezwa na