Sera ya Faragha
Benki ya CRDB, ni benki ya biashara iliyoundwa mwaka 1996. Benki iliorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) mwezi Juni 2009. Kwa sasa ina kampuni tanzu nne, CRDBBank Burundi (S.A), CRDB Bank Congo S.A, CRDB Insurance Company Limited na CRDBFoundation.
Benki imejidhatiti kulinda taarifa zako binafsi pamoja na kuhakikisha kiwango cha juu kabisa cha usalama wa taarifa zako. Sera hii ya taarifa binafsi inaeleza aina za taarifa tunazokusanya, jinsi tunavyotumia taarifa, na tunasambaza wapi, na jinsi tunavyolinda taarifa hizo. Pia inatoa taarifa kuhusu haki zako.
Tafadhali soma kwa uangalifu ili kuelewa taratibu zetu kuhusu uchakataji wa taarifa zako binafsi.
- Sisi ni nani?
Kulingana na bidhaa na huduma zetu ambazo unazoziulizia, unazonunua au unazotumia, kampuni zetu tanzu ndani ya shirika letu zitachakata taarifa zako. Kwa ujumla, Benki imejidhatiti kuunda bidhaa na huduma ambazo kwanza zinazingatia mahitaji ya wateja. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanakuwa na amani na uhakika tunapowasaidia kupata suluhisho bora kwa ajili yao ili waweze kufanya kazi vizuri zaidi.
- Wigo wa Sera ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi
Taarifa binafsi zinatumika kwa mtu yeyote aliye ndani au nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye anaulizia, kununua au kutumia bidhaa na huduma zetu zinazotolewa na Benki.
- Njia tunazotumia kupata Taarifa Binafsi
Tunaweza kukusanya taarifa zako kutoka vyanzo vifuatavyo:
a). Taarifa tunazopokea kutoka kwako
Tunapata taarifa binafsi zinazokuhusu kupitia mawasiliano baina yako na sisi, ikiwa ni pamoja na kupitia njia ya simu (ambazo zinaweza kurekodiwa na utajulishwa kabla ya kurekodiwa), kwa barua pepe, kupitia tovuti zetu, kupitia App (SimBanking) au fomu nyingine au ana kwa ana(k.m. katika mikutano). Tunakusanya taarifa za binafsi (kama vile jina lako, maelezo ya mawasiliano, taarifa za kifedha, taarifa ya ajira na elimu, uraia, tarehe na mahali pa kuzaliwa, hali ya ndoa, pasi ya kusafiria au taarifa nyingine za utambulisho na taarifa nyinginezo unapotelembelea ofisini kwetu) ambazo unatupatia wakati unapo:
i). Ulizia kuhusu bidhaa na huduma zetu;
ii). Wasilisha maombi ya kufungua akaunti na
iii). Na kufanya mawasiliano nasi baadaye.
b). Taarifa zako tunazokusanya
Tunakusanya taarifa zako pale unapofika ofisini kwetu kupitia mifumo yetu ya ulinzi (kama CCTV). Pia tunakusanya taarifa zako kutoka kwenye tovuti yetu, ikiwa ni pamoja na anuani ya mtandao (IP Address) au taarifa nyingine za vifaa vya mtandao (utaona habari zaidi kuhusu hii katika taarifa yetu ya vifaa vya mtandao kama simu za mkononi).
c). Habari tunazopokea kutoka kwa watu wengine
Tunapokea taarifa zinazokuhusu kutoka kwa watu wengine (kama taasisi zinazotoa taarifa kuhusu wakopaji).
- Tunatumiaje taarifa zako Binafsi?
Tunatumia taarifa zako binafsi kwa madhumuni yaliyoelezwa hapa. Misingi tofauti ya kisheria inatumika kulingana na aina ya taarifa binafsi zilizopo. Taarifa binafsi za kawaida hutumiwa na sisi kwa msingi ya kwamba ni muhimu katika utekelezaji wa mkataba, maslahi yetu au maslahi halali ya mnufaika mwingine au sheria. Kwa maelezo zaidi kuhusu hii na misingi ya kutumia makundi maalum ya taarifa yanapatikana hapa chini.
Tunatumia taarifa zifuatazo: |
Kwa madhumuni yafuatayo: |
Kulingana na sababu zifuatazo: |
Jina, Namba ya Kitambulisho, Uraia, Taarifa za Pasipoti, Maelezo ya Kodi, Tarehe ya Kuzaliwa, Mahali pa Kuzaliwa, Anuani ya Makazi, Anuani ya Biashara, Kazi, Saini, Historia ya Ajira, Taaluma, Taarifa za Kifedha, Rekodi za Jinai |
Ili kurahisisha mchakato wetu wa kufungua akaunti, mchakato wetu wa kumfahamu mteja, na mchakato wetu wa kumfahamu muuzaji, pamoja na kuzuia udanganyifu na matumizi mabaya ya huduma zetu. |
Ni muhimu kutekeleza mkataba wetu, kuzingatia mahitaji yetu ya kisheria, na kwa ujumla ili kufuatilia maslahi yetu halali (ona hapa chini) ya kusimamia shughuli zetu za utawala na biashara na kuzingatia sera na taratibu za ndani. |
Taarifa za Kifedha na Miamala (kwa mfano, maelezo kuhusu akaunti zako nasi na malipo kutoka na kwenye akaunti zako nasi) |
Ili kutuwezesha kuhifadhimiamala yako. Kutekeleza taratibu zetu za Ripoti za Kisheria na kurahisisha kushughulikia na kuripoti kesi za udanganyifu (pale inapohitajika). |
Ni muhimu kutekeleza mkataba wetu na kuzingatia mahitaji yetu ya kisheria, na kwa ujumla ili kufuatilia maslahi yetu halali (angalia hapa chini). |
Simu |
Ufuatiliaji wa shughuli zilizodhibitiwa, mafunzo na maendeleo. |
Kuzingatia mahitaji yetu ya kisheria na kufuatilia maslahi yetu halali (angalia hapa chini) ya kuboresha ubora wa huduma zetu. |
Maelezo ya malalamiko yoyote |
Ili kurahisisha kushughulikia malalamiko na kuripoti. |
Ili kuzingatia mahitaji yetu ya kisheria. |
- Maslahi Halali
Maslahi halali ni moja ya sababu za kisheria kwa nini tunaweza kuhifadhi taarifa zako binafsi. Tunahifadhi taarifa zako binafsi kwa ajili ya maslahi halali kadhaa, ikiwa ni pamoja na kusimamia vipengele vyote vya uhusiano kati yetu na wewe, kwa ajili ya masoko, kutusaidia kuboresha huduma na bidhaa zetu, na ili kutumia haki zetu au kushughulikia madai. Kwa kuzingatia maslahi yako, haki zako, na uhuru wako, maslahi halali ambayo yanaturuhusu kuhifadhi taarifa zako binafsi ni pamoja na:
a) Kusimamia uhusiano baina yetu, biashara yetu na watu wengine wanaotoa bidhaa au huduma kwa niaba yetu;
b) Kuhakikisha kuwa malalamiko au maswali yanashughulikiwa kwa ufanisi na kuboresha bidhaa na huduma zetu;
c) Kusanikisha rekodi zetu na kukupa masoko kama inavyoruhusiwa kisheria;
d) Kukuza na kutekeleza shughuli za masoko na kukupa taarifa unazopendelea, kulingana na ufahamu wetu wa kile unachopendelea;
e) Kufuatilia jinsi tunavyotimiza matarajio yetu ya utendaji katika utoaji wa huduma zetu (k.m., rekodi za simu);
f) Kufuatilia maslahi yetu halali katika kusimamia usalama wa mazingira yetu na huduma kwa kuzuia, kugundua na kufuatilia uhalifu, afya ya usalama (k.m., picha za video za CCTV);
g) Kutekeleza au kutumia masharti ya matumizi ya tovuti yetu, masharti na hali ya sera zetu au mikataba mingine, au kulinda haki, mali au usalama wetu (au wateja wetu au wadauwengine);
h) Kutumia haki zetu, kujilinda kutokana na madai na kuzingatia sheria na kanuni zinazotuhusu sisi na watu wengine tunaofanya nao kazi; na
i) Kushiriki katika, au kuwa mada ya, ununuzi, mauzo, muungano au unyakuzi wa sehemu au sehemu zote za biashara yetu.
- Je! Tunatumia taarifa zako binafsi kwa ajili ya masoko?
Kwa idhini yako, tunaweza kukutumia taarifa iliyochaguliwa kwa umakini kuhusu bidhaa na huduma zetu. Una haki ya kujiondoa kutoka kwa kupokea taarifa za masoko wakati wowote kwa kuwasiliana nasi kupitia wakala wetu wa huduma kwa wateja.
- Tunatuma taarifa zako binafsi kwa watu gani?
Tunatuma taarifa yako kwa madhumuni yaliyoelezwa katika sera hii ya ulinzi wa taarifa binafsi, na makundi yafuatayo ya wapokeaji:
a. Kampuni tanzu za Benki: Tunatuma taarifa yako ya kibinafsi kwa kampuni tanzu za Benki yetu, ikiwa ni pamoja na matawi yetu (ndani na nje ya nchi) ili kufungua akaunti yako, kusimamia huduma na bidhaa zetu, kukupa msaada wa wateja, kufanikisha malipo yako, kuelewa machaguo yako, kukutumia taarifa kuhusu bidhaa na huduma ambazo zinaweza kukuvutia, na kufanya shughuli nyingine zilizoelezwa katika Taarifa hii.
b. Watoa huduma wetu: Tunatumia makampuni mengine, mawakala au wakandarasi kutekeleza huduma kwa niaba yetu au kutusaidia katika utoaji wa huduma na bidhaa zetu kwako, ikiwa ni pamoja na:
i. Watoa huduma wa miundombinu na huduma za IT, pamoja na kuhifadhi barua pepe.
ii. Mashirika ya masoko, matangazo na mawasiliano.
iii. Mashirika ya kumbukumbu ya mikopo
iv. Wakaguzi wa nje na washauri
v. Wakati wa kutoa huduma hizo, watoa huduma hawa wanaweza kufikia taarifa zako binafsi. Hata hivyo, tutatoa kwa watoa huduma wetu taarifa hiziambazo ni muhimu kwao kutekeleza huduma zao, na tunawahitaji wasitumie taarifa zako kwa madhumuni mengine yoyote. Tutatumia jitihada zetu bora kuhakikisha kuwa watoa huduma wetu wote wanahifadhi taarifa zako kiusahihi na kiusalama.
c. Wapokeaji wengine walioruhusiwa na sheria: Katika hali fulani, tunaweza kulazimika kufichua au kutuma taarifa zako binafsi ili kuzingatia jukumu la kisheria (kwa mfano, tunaweza kulazimika kufichua taarifa zako binafsi kwa polisi, wasimamizi, mashirika ya serikali, mahakama au mamlaka yoyote ya kiutawala ambayo yamepewa mamlaka na sheria kutafuta taarifa hiyo).
i. Pia tunaweza kufichua taarifa zako binafsi kwa wapokeaji wengine ambapo ufichuaji wa taarifa ni halali na muhimu kwa kusudi la kulinda au kutetea haki zetu, masuala ya usalama wa taifa, kutekeleza sheria, kutekeleza mikataba yetu au kulinda haki zako au za umma.
d. Wadau wengine watakaojihusisha na kusambaza taarifa: Tunaweza kusambaza taarifa zako binafsi kwa wadao wengine wanaohusika na mabadiliko kama vile ya kampuni au muundo, muungano, ununuzi au uhamishaji wa mali, ikiwa upande wa mpokeaji unakubaliana kutumia taarifa zako binafsi kwa njia inayolingana na taarifa hii.Hatutauza taarifa yako ya kibinafsi kwa watu wengine.
- Haki zako ni zipi?
Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawapa watu binafsi haki zifuatazo:
a) Haki ya kupata maelezo ya taarifa za binafsi: Haki ya kuomba kwa maandishi maelezo ya taarifa binafsi kuhusu wewe na kuomba nakala ya taarifa hizo.
b) Haki ya marekebisho: Haki ya kuwa na taarifa zisizo sahihi kuhusu wewe zirekebishwe.
c) Haki ya kufutwa: Haki ya kufutwa kwa baadhi ya taarifa binafsi kuhusu wewe.
d) Haki ya kuzuia mchakato wa taarifa: Haki ya kuomba taarifa zako binafsi zitumike tu kwa madhumuni fulani.
e) Haki ya kupinga: Haki ya kupinga matumizi ya taarifa binafsi (ikiwa ni pamoja na haki ya kupinga masoko).
f) Haki ya kuhamisha taarifa: Haki ya kuomba taarifa binafsi ulizotoa kwetu zipelekwe kwako au kwa mtu mwingine.
g) Haki ya kujiondoa: Una haki ya kujiondoa kwa idhini yoyote uliyotupa kushughulikia taarifa zako binafsi. Ikiwa utajiondoa kwa idhini yako, hii haitaathiri uhalali wa matumizi ya taarifa zako binafsi kabla ya kujiondoa kwa idhini yako.
Haki hizi zinategemeana na mazingira ya kila ombi utakaloleta kulingana na matakwa ya sheria zingine. Ikiwa hatuwezi kutekeleza ombi lako, tutaeleza kwanini. Kujibu ombi, tutakuuliza uhakiki wa utambulisho wako ikiwa ni lazima, na kutoa maelezo ambayo yatasaidia kuelewa ombi lako vizuri zaidi. Ikiwa ungependelea kupata maelezo zaidi kuhusu haki zako au utumiaji wa haki zako yoyote, tafadhali wasiliana kwa barua pepe: [email protected]
Pia una haki ya kuwasilisha malalamiko kwa tume ya ulinzi wa data ya binafsi, ikiwa unaamini kwamba hatujazingatia sheria husika za ulinzi wa data.
- Tunalinda vipi taarifa yako ya kibinafsi?
Tumetekeleza udhibiti wa kiufundi kwa ajili ya kuhifadhi taarifa ya binafsi katika ulinzi na udhibiti wetu. Hatua kama hizo ni pamoja na, kwa mfano:
▪ Kupunguza ufikiaji wa taarifa ya binafsi kwa wafanyakazi na watoa huduma walioidhinishwa ambao wanahitaji kujua taarifa hizo kwa madhumuni yaliyoelezwa katika taarifa hii;
▪ Kuchukua itifaki imara za usalama kwenye mitandao na mifumo;
▪ Kutumia mipangilio ya usalama wa barua pepe wakati wa kutuma na/au kupokea barua pepe za siri;
▪ Kupunguza udhibiti wa ufikiaji kama vile kuweka alama kwenye nyaraka za siri kwa njia ya vidole, kizuizi cha ufikiaji wa nyaraka za siri;
▪ Kuchuja taarifa binafsi
▪ Kuondoa nyaraka za siri ambazo hazihitajiki tena, kwa kutumia vifaa husika;
▪ Kutumia njia ya utoaji au uhamishaji wa taarifa binafsi inayotoa kiwango sahihi cha usalama, kuthibitisha mpokeaji aliyelengwa pamoja na ulinzi mwingine wa kiutawala, kiufundi.
Ingawa tunajitahidi kulinda mifumo yetu, tovuti, shughuli na taarifa dhidi ya ufikiaji usio halali, matumizi, mabadiliko na ufichuaji, kutokana na asili ya mtandao kama njia ya mawasiliano ya kimataifa na mambo mengine ya hatari, hatuwezi kuhakikisha kwamba taarifa yoyote, wakati wa usafirishaji au wakati iliyohifadhiwa kwenye mifumo yetu, itakuwa salama kabisa kutoka kwa kuingiliwa na wengine, kama vile wadukuzi.
- Tunahifadhi taarifa zako binafsi kwa muda gani?
Tutahifadhi taarifa zako binafsi kwa muda tu unaohitajika kwa kusudi ambalo taarifa hiyo ilikusanywa na kwa kiwango linaloruhusiwa na sheria husika.
- Unawezaje kuwasiliana nasi?
Ikiwa kuna maswali au wasiwasi wowote kuhusu taarifa binafsi, tafadhali wasiliana nasi kama ifuatavyo: Barua pepe: [email protected]
- Taarifa ya vifaa vya mtandao (Cookies)
Ili kukidhi matarajio ya wateja na kuboresha huduma zinazotolewa kwenye tovuti yetu, tunatumia taarifa ya vifaa vya mtandao. Kwa kufikia tovuti ya benki, umekubali kutumia taarifa ya vifaa vya mtandao kwa mujibu wa sera ya ulinzi wa taarifa ya benki ya CRDB inayopatikana kwenye tovuti ya benki.
Tovuti nyingi zenye mwingiliano hutumia taarifa ya vifaa vya mtandao kuruhusu kupata maelezo ya mtumiaji kila anapotembelea tovuti. Taarifa ya vifaa vya mtandao hutumiwa na tovuti yetu kuwezesha utendaji wa maeneo fulani ili kuifanya iwe rahisi kwa watu wanaotembelea tovuti yetu. Kwa kukubali masharti haya, pia unakubaliana na washirika/waandishi wa matangazo wetu ambao pia wanaweza kutumia taarifa ya vifaa vya mtandao.
a) Taarifa ya vifaa vya mtandao ni nini?
Ni faili ndogo la maandishi lilizohifadhiwa kwenye kifaa chako cha kompyuta au vifaa vingine vya kielektroniki ambavyo vinaturuhusu kukukumbuka au kuhifadhi taarifa nyingine kuhusu wewe. Taarifa ya vifaa vya mtandao iliyowekwa na seva yetu inaweza kusomwa tu na sisi, na haiwezi kufikia, kusoma au kubadilisha taarifa nyingine yoyote kwenye kifaa cha kielektroniki. Wavuti hutoa chaguo la kukataa taarifa yoyote ya vifaa vya mtandao, na ikiwa unakataa basi hatutakusanya habari yoyote kuhusu wewe.
b) Matumizi ya Taarifa ya vifaa vya mtandao ni yapi?
Taarifa ya vifaa vya mtandao hutumiwa kwa madhumuni mbalimbali. Tunaweza kutumia ili seva yetu itambue mgeni anayerudi kama mtumiaji wa kipekee, ikiwa ni pamoja na, bila kikomo, kufuatilia habari inayohusiana na jinsi mgeni anavyofika kwenye tovuti, aina ya kivinjari ambacho mgeni anatumia, mfumo gani wa uendeshaji ambao mgeni anatumia, anuani ya IP ya mgeni, na muda na taarifa ya mzunguko wa mgeni (kwa mfano, ni kurasa zipi wamezitembelea, muda wa kurasa zilizofikiwa na muda uliotumiwa kwa kila ukurasa wa wavuti).
c) Ni aina gani za Taarifa ya vifaa vya mtandao tunazotumia?
Tunatumia Taarifa ya vifaa vya mtandao kulingana na Lengo: ambavyo hukusanya taarifa kuhusu tabia yako ya kuvinjari ili kufanya matangazo yanayohusiana na wewe na maslahi yako.
d) Chaguzi zako ni zipi?
Ikiwa ungependa kusitisha taarifa ya vifaa vya mtandao vinavyohusiana na teknolojia hizi, unaweza kufanya hivyo Kwa kubadilisha mipangilio.
Ikiwa una maswali, mapendekezo, au maoni kuhusu taarifa hii ya vidakuzi, tuma barua pepe kwa [email protected].
Sera yetu ya ulinzi wa taarifa binafsi na Taarifa ya vifaa vya mtandao inaweza pia kubadilishwa mara kwa mara, kwa hivyo tembelea ukurasa huu kwa ukawaida ili kujua mabadiliko.
Unaweza kupendezwa na
Taarifa
Soma ZaidiProduct Terms and Conditions
These terms and conditions outline the rules and regulations for the use of the bank’s website located at www.crdbbank.co.tz
Soma ZaidiTerms and Conditions for Simbanking App
Terms and Conditions outline the rules and regulations for using Simbanking App
Soma ZaidiVigezo na Masharti
Vigezo na masharti haya yanaainisha sheria na kanuni za matumizi ya tovuti ya benki iliyopo www.crdbbank.co.tz
Soma Zaidi