Work With Us
Kwa nini ufanye kazi nasi?
Sisi ni mkusanyiko wa watu ambao wanaamini ubora. Daima tunatafuta talanta mpya na tunaajiri watu ambao wana hamu ya kufanikiwa na nia ya kutekeleza nidhamu inayohitajika kufanikiwa. Tunazingatia kukuza vipaji na kuipatia timu yetu mazingira ambayo yanafaa kwa mawazo ya ubunifu.
Kazi katika Benki ya CRDB inakupa fursa ya kuwa na katika taasisi inakuyokua kwa kasi Afrika.
Hizi ndio sababu CRDB ni pahali pazuri pa kufanyia kazi
1. Chapa yetu inajulikana
Tuna urithi mkubwa kama chapa ya Kiafrika iliyotengenezwa nchini Tanzania. Tuna historia ndefu ya miaka 25 na hadithi yetu inajikita katika maendeleo na kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kujenga maisha endelevu kwa wateja wetu. Tunaamini katika fadhila za Kiafrika za wema na roho ya ustahimilivu. Maono yetu ya muda mrefu ni kuleta mabadiliko chanya katika masoko yetu yote kupitia uvumbuzi wa sekta ya fedha na kuwa wachochezi wa mageuzi katika sekta hiyo.
2. Watu Wahamasishaji
Moja ya nguvu zetu kubwa ni watu wetu na nia yetu ya pamoja ya kujenga mazingira jumuishi ambamo kila mtu anathaminiwa na kila sauti inasikilizwa. Utamaduni wetu umejikita katika maadili ya kampuni yetu. Tunakuza mazingira ya ujumuishi, umiliki na usawa kwa wote ili kujenga mahali pa kazi bora, kuendeleza uvumbuzi sokoni na matokeo chanya katika jamii zetu. Tunajitahidi kuwa chaguo la waajiriwa ili kuleta manufaa ya huduma zetu kwa wote.
3. Tamaduni Mbalimbali na Jumuishi
Tunapenda kukusanya pamoja watu wanaotoka sehemu mbalimbali, wenye talanta na asili tofauti. Tunanufaika kutokana na mawazo tofauti ambayo kila mmoja wetu huleta na kwa pamoja tunatumia vipaji hivi kuwa kiongozi katika sekta ya fedha.
4. Kujitoa kwa Uendelevu
Tumejitolea kujiendesha kama zaidi ya benki - kwa manufaa ya wote. Fikra zetu na ubunifu wetu unaenda mbali zaidi ya huduma tunazotoa. Inafikia hadi jinsi tunavyozitengeneza na wale tunaowatengenezea.
5. Fursa za Kukua
Unapofanikiwa, CRDB inafanikiwa. Benki ya CRDB inatoa zana mbalimbali za kusaidia maendeleo shirikishi kama vile mabadiliko, ushauri, mafunzo ya kiutendaji na kujenga timu.
6. Kitengo Maalum cha Kujifunza na Maendeleo
Kuendeleza wafanyikazi wetu ni moja ya mikakati muhimu kwetu na tunaupa kipaumbele. Tuna Kitengo chetu cha Kujifunza na Maendeleo ambacho hutoa zana na fursa za kujifunza zinazowawezesha wafanyakazi kujiwekea malengo madhubuti yao na timu zao ili kukabiliana na changamoto mpya. Ni mbinu ya kujifunza inayojumuisha: Kozi za Darasani, Kozi za Mtandaoni na Ukuzaji wa Uongozi. Kituo cha Mafunzo cha Benki kimekuwa ISO 9001.
7. Faida Kwa Ajili Yako
Hapa CRDB, tunatoa fidia shindani na manufaa mbalimbali ambazo husaidia kufanya maisha na afya yako kuwa rahisi. tukilenga kukupa chaguo kwenye suala la ustawi wa kimwili, kihisia na kifedha. Chaguzi zetu hukutana na wewe ulipo katika maisha yako na kukutayarisha kwa ajili ya mafanikio ndani na nje ya mazingira ya kazi.
TUNAKUSUBIRI. KAZI UNAYOITAFUTA IKO KARIBU.
KARIBU CRDB BANK.
(Maombi yote na mahojiano yatafanywa kwa Kiingereza)
Katika mchakato wa kushughulikia wawezeshaji, benki kupitia Idara yake ya Rasilimali Watu imekuwa ikifanya maonesho ya ajira kama moja ya Youth Proposotion Initiative kwa lengo la kuandaa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kuwa na ustadi unaohitajika katika soko la ushindani wa kazi na kufanikisha mipango ya benki inayolenga kujenga nguvu kazi yenye ujuzi ndani na nje ya nchi.
Maonesho ya Ajira ni hafla inayoleta pamoja benki na wafanyakazi wanaotarajiwa yani wanafunzi na wanaotafuta kazi katika mazingira yasiyo rasmi na unganishi. Kupitia hafla hii vijana huchunguza chaguzi zao za kazi na pia hutumia jukwaa hilo kukuza uwezo wao utaohitajika katika ulimwengu wa ushindani na utandawazi.
Career Fair imekuwa moja ya majukwaa muhimu yanayotumika na makampuni kuonesha nafasi yao sokoni na kama waajiri.
Idara ya Rasilimali watu inashirikiana na mashirika mengi, kama AIESEC na Taasisi ya uhasibu Tanzania - Singida katika maandalizi na kutumia jukwaa hili kama fursa moja wapo za biashara zinazoleta wateja vijana karibu na CRDB. Shughuli ambazo hufanyika wakati wa maonesho ya taaluma, bidhaa za benki na maonesho ya maendeleo ya ujuzi na maswali ya wasomi.
Safari yako ya ajira inaanza hapa. Tukutane Career Fair 2022 pale Chuo cha Uhasibu Singida, Jumamosi Tar 28 Januari, upate maelezo zaidi kuhusu sekta ya fedha na uongozi.
Jiandikishe sasaMaswali