Nini Kipya??
VIEW ALL

Maswali

CRDB Bank inaendesha Kampeni ya Lipa Hapa, yenye lengo la kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidijitali kupitia mfumo wa CRDB Lipa Hapa kwa wafanyabiashara na wateja wake. Kampeni hii itaendeshwa kwa kipindi cha Machi 2026 hadi Desemba 2026.                   

Kupitia kampeni hii, wafanyabiashara wa CRDB watapata fursa ya kujishindia zawadi ya fedha taslimu kwa kila muamala unaofanyika kupitia Lipa Hapa ya CRDB, kutoka kwa wateja wa CRDB Bank.

Kwa kila malipo ya bidhaa au huduma yatakayofanyika kupitia Lipa Namba ya CRDB, mfanyabiashara atazawadiwa shilingi mia tano (500) kwa kila muamala ulioanzia shilingi elfu kumi (10,000) na kuendelea.

Zawadi hii itahesabiwa kulingana na idadi ya miamala halali iliyofanyika katika kipindi husika cha mwezi.

Ili muamala kuhesabika kwenye kampeni hii, ni lazima:                                               

  • Mteja awe ni mmiliki wa akaunti ya CRDB Bank
  • Malipo yafanyike kupitia mfumo wa CRDB Lipa Hapa
  • Kiasi cha muamala kiwe shilingi elfu kumi (10,000) au Zaidi
  • Muamala ufanyike ndani ya kipindi cha kampeni (Machi–Desemba 2026)
                           

Note: Ni miamala ya wateja wa CRDB pekee itakayohesabiwa katika kampeni hii.

  • Miamala yote ya CRDB iliyopita kupitia Lipa Hapa ya CRDB itakusanywa kila mwisho wa mwezi.
  • Jumla ya miamala halali itazidishwa na shilingi mia tano (500).
  • Kiasi kilichopatikana ndicho kitakacholipwa kwa mfanyabiashara.
  • Malipo yatafanyika kila mwisho wa mwezi moja kwa moja kwenye akaunti ya mfanyabiashara.

  • Kuongeza matumizi ya malipo ya kidijitali
  • Kuongeza mzunguko wa miamala 
  • Kupata zawadi ya pesa taslimu kila mwezi 
  • Kuimarisha ushirikiano na CRDB Bank