Benki ya CRDB yawakaribisha Watanzania kuchangamkia mikopo miradi inayolinda mazingira

By: Niels Malangalila | Blog | Septemba 9, 2025 05:44

Benki ya CRDB yawakaribisha Watanzania kuchangamkia mikopo  miradi inayolinda mazingira

Katika mkakati wa kuendeleza juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, Benki ya CRDB imezindua mikopo mahsusi kwa ajili ya miradi na biashara zinazolinda mazingira. Mikopo hiyo mahsusi inayotambulika kwa jina la Mikopo ya KIJANI imezinduliwa na Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa mbele ya wadau wanaoshiriki kuiwezesha jamii kutekeleza miradi inayokusudia kuleta uendelevu wa kijamii na mazingira.

“Mwaka 2023, Benki yetu ya CRDB ilitoa Hatifungani ya Kijani iliyoorodheshwa Soko la Hisa Dar es Salaam na Soko la Hisa la Luxembourg na kuuzwa kwa mafanikio yaliyo iwezesha Benki kukusanya jumla ya shilingi bilioni 171.82. leo ninayo furaha kuwakaribisha wanyabiashara na wajasiriamali wenye miradi inayolinda kupata fedha zitakazowawezesha kuitekeleza kwa mafanikio miradi yao,” amesema Raballa. Fedha hizo, Raballa amesema fedha hizi zitajikita zaidi katika sekta zifuatazo zenye kuleta tija kwa wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs): i. Mikopo ya Angaza - kuwezesha matumizi ya nishati ya jua na kuleta mabadiliko katika sekta za elimu, afya, biashara mahoteli, uzalishaji wa viwandani na biashara na mafuta na gesi. ii. Mikopo ya Nishati Safi – kuwezesha katika matumizi ya nishati safi ya kupikia katika sekta ya elimu mahoteli, kubadilisha miundombinu ya kupikia katika shule, viwanda, na hoteli kwa kutumia vifaa vinavyotumia LPG, biogesi, na umeme kwa ufanisi wa nishati na vifaa vinavyotumia nishati kwa ufanisi — jokofu, vyumba vya baridi, viyoyozi n.k. iii. Mikopo ya ukusanyaji na uchakataji taka ikilenga biashara za uchakataji wa taka wasanii wa uchakataji wa taka. iv. Mikopo ya Usafiri Safi kuwezesha sekta ya usafiri kwa usafiri safi na rafiki kwa mazingira. Uzinduzi wa mikopo hii kwa miradi na biashara zinazolinda mazingira, Raballa amesema ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa Benki ya CRDB wa kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuchochea miradi ya nishati mbadala, kilimo endelevu, biashara ndogo na za kati, pamoja na miradi ya kijamii inayochangia kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa. “Katika mpango huu tunalenga kuwawezesha Watanzania zaidi ya milioni 2 kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na kuhamia kwenye nishati mbadala kama vile umemejua, majiko banifu, na mifumo ya nishati jadidifu ili kulinda misitu, kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa, kuboresha afya na kukuza uchumi wa kijani. Tayari tumeshaanza utekelezaji katika mikoa kadhaa na matarajio yetu ni kupanua huduma hizi nchi nzima ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo,” amesema Raballa. Raballa amefafanua kwamba tayari baadhi ya wateja wa Benki ya CRDB wameshaanza kunufaika na fedha hizi ambao ni wale ambao walileta maombi yao siku nyingi na mpaka sasa Benki yetu ya CRDB imeshatoa zaidi ya shilingi bilioni 157 kwenye miradi iliyokidhi vigezo ikiwamo ya kilimo, nishati na maeneo. “Tunatambua changamoto zinazowakabili wajasiriamali, hususan upatikanaji wa mitaji nafuu na ujuzi wa uendeshaji wa biashara. Kwa msingi huo, tumeweka masharti nafuu ya mikopo, muda mrefu wa urejeshaji unaoendana na uhalisia wa biashara zao, pamoja na huduma za kujenga uwezo kupitia mafunzo ya ujasiriamali, usimamizi wa fedha na matumizi ya teknolojia bunifu ili kuwashika mkono wajasiriamali hawa kuanzia hatua za mwanzo za ukuaji wao kiuchumi. Benki ya CRDB tunaamini maendeleo ya kiuchumi lazima yaendane na ulinzi wa mazingira,” ameeleza Raballa. Hatifungani ya Kijani ni awamu ya kwanza ya Mpango wa Muda wa Kati wa miaka mitano unaolenga kukusanya shilingi bilioni 780 sawa na dola za Marekani milioni 300. Benki ya CRDB ndio taasisi pekee ya fedha nchini na ya kwanza kusini mwa Jangwa la Sahara kusajiliwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UN-GCF) ulioiwezesha kupata dola za Marekani milioni 100 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kilimo kinachozingatia utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kupitia programu ya TACATDP yaani Tanzania Agriculture Climate Adaptation Technology Deployment Programe ambao benki inachangia dola milioni 100 na kuufanya kuwa na thamani ya dola milioni 200. Katika utekelezaji wa programu hii, Benki ya CRDB inashikiriana na IFC, kampuni tanzu ya Benki ya Dunia kuhakikisha Watanzania wanaungana na wananchi wa ulimwengu mzima kuilinda dunia na viumbehai vilivyomo. Mkurugenzi Mkazi wa IFC nchini, Martine Valcin amesema ongezeko la shughuli za uzalishaji umeongeza mahitaji ya rasilimali tofauti ambazo uvunaji wake mkubwa unaathiri mazingira ndio maana ni muhimu kwa watu wote duniani kishirikiana kuyalinda.

What's new?

CRDB Bank's Second Africa Investment Forum in Bangkok Successfully Advances Global Investment Partnerships for Africa's Growth

BLOG

CRDB Bank's Second Africa Investment Forum in Bangkok Successfully Advances Global Investment Partnerships for Africa's Growth

...

Read More: CRDB Bank's Second Africa Investment Forum in Bangkok Successfully Advances Global Investment Partnerships for Africa's Growth
Tanzania Shines on the Global Stage as CRDB Bank and Bank of Tanzania Honoured by Global Finance

BLOG

Tanzania Shines on the Global Stage as CRDB Bank and Bank of Tanzania Honoured by Global Finance

...

Read More: Tanzania Shines on the Global Stage as CRDB Bank and Bank of Tanzania Honoured by Global Finance
CRDB Bank Goes “The Extra Mile” with an enhanced SimBanking

BLOG

CRDB Bank Goes “The Extra Mile” with an enhanced SimBanking

...

Read More: CRDB Bank Goes “The Extra Mile” with an enhanced SimBanking